Habarini wapendwa. Naomba msaada kwa wanachama wenye uelewa na huu mfuko wa kijamii wa LAPF. Ni hivi, si muda mrefu (wiki 2) toka Mke wangu ajifungue! Tumekuwa tukijiuliza kila leo endapo kuna fungu (pesa) la mzazi ndani ya mfuko huu kwa wanachama. Mke wangu ni mwanachama kwa miaka 3 sasa. Lengo ni kupata haki za mwanachama. Pesa za kumlea mama na mtoto ninazo (maana najua wengine mtakuja na mitazamo tofauti). Msaada kwa waelewa tafadhaki. Ahsanteni!