Msaada kwa wana NSSF

Msaada kwa wana NSSF

Jodeo

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2015
Posts
1,286
Reaction score
1,332
Natumai hamjambo wote mliofunga na msiofunga.

Naomba kujuzwa kwa wanaofahamu, nilikuwa nafanya kazi na kampuni moja huku Mwanza ambayo makao makuu yapo Dar.

Baada ya kuacha kazi nimejaribu kufuatilia mafao nikiwa huku Mwanza, maofisa wa NSSF wakanambia kwa kuwa michango yangu ilikuwa ikiwekwa tawi la Temeke inabidi nifungue madai Temeke na siyo Mwanza.

Swali: Huu utaratibu ndiyo wenyewe au vipi? Na NSSF kama mnaisoma hii thread kwa nini mmeweka utaratibu uchwara namna hii ( kama ni kweli)?

Naomba msaada wenu kama hii procedure iko sawa.
 
Asalam aleykum, bila shaka wewe ulikua ukifanya kazi barrick(acacia) ndo wenye ofisi dar msasani peninsula, kwa msaada tu, mm nimetoka kuchukua nssf mafao last week, ni kwamba kila kampuni huwa inapitisha michango kwa tawi la nssf walilochagua wao, kwa mf.
 
Kwa mf. Mm nilikuwa nafanya kazi songea, lakini mafao yangu yalikua yanapitia nssf tawi la mlimani city, wasiliana na mwajili wako wa awali akwambie michango yako ilikuwa ikipitishiwa nssf branch ipi. Na utaratibu kampuni 90% wanatuma michango miez 3 mitat
 
pole ndugu, yote tisa sawa, lakini hili la uchwara, naona kama unawapa hadhi ambayo si stahiki! nipo nao mwaka sasa kama mwanachama wa hiari, nssf mambo yao kwa mtazamo wangu, kama bima yao ya afya naona safi sana.
 
Asante mkangaf,,, michango Yangu ilipitiahwa tawi la temeke. Sasa ili kupata mafao ni lazima niende dar? ( temeke) kama walivyonielekeza maofisa wao hapa mwanza?
 
Back
Top Bottom