Msaada kwa walio kwenye uchumba na wazoefu

bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,383
1,354
Ninarafiki yangu ametoa mahari mwanzoni mwa mwaka huu na anategemea kuoa early June this year ila kuna kitukimoja kinamtatiza sana nacho ni wakati gani unafaa kwa yeye na mchumba wakekupeana passwords na username zao zamitandao yote ambayo amejiunga mfono yahoo, gmail, skype na facebook na pia niwakati gani mwafaka kwa hawa wachumba wanapaswa kuelezana akiba zao zilizopokwenye mabenk. Msaada wenu wa muongozo unahitajika
 
luk mie naona kama kashafika stage ya kutoa mahari na kupanga harusi anaweza kumwambia tuu kwani yeye anaficha nini mpaka anaogopa kumwambia???
 
Talking from experience,kupeana mi passwords ni kujitafutia mitafaruku isiyo na maana.Mnapendana ndiyo,thats fine,but you still need some privacy.
 
I dont think this should be an issue kwenye mahusiana yao, when the time comes watajua tu na watapeana.
Hata ivyo ukishajua PW ya mtu itakusaidia nini?
 
Suala la nywila zangu FB,JF,Gmail linahusika vipi? kila mtu abaki na zake bana..presha zingine watu hua wanajitakia wenyewe
 
Ninarafiki yangu ametoa mahari mwanzoni mwa mwaka huu na anategemea kuoa early June this year ila kuna kitukimoja kinamtatiza sana nacho ni wakati gani unafaa kwa yeye na mchumba wakekupeana passwords na username zao zamitandao yote ambayo amejiunga mfono yahoo, gmail, skype na facebook na pia niwakati gani mwafaka kwa hawa wachumba wanapaswa kuelezana akiba zao zilizopokwenye mabenk. Msaada wenu wa muongozo unahitajika

Wanataka kupeana password za nini? Basi kwa namna moja ama nyingine hawaaminiani
 
Hakuna wakati maalum wa kufanya hivyo. Kwenye vitabu vya kanuni hiyo haipo.
 
Toka lini ameambiwa hilo ni sharti ama lazima? Ama vituko duniani havitaisha!
 
Ninarafiki yangu ametoa mahari mwanzoni mwa mwaka huu na anategemea kuoa early June this year ila kuna kitukimoja kinamtatiza sana nacho ni wakati gani unafaa kwa yeye na mchumba wakekupeana passwords na username zao zamitandao yote ambayo amejiunga mfono yahoo, gmail, skype na facebook na pia niwakati gani mwafaka kwa hawa wachumba wanapaswa kuelezana akiba zao zilizopokwenye mabenk. Msaada wenu wa muongozo unahitajika

Ndugu yangu inakubidi uielewe ndoa vizuri, sivyo kama unavyofikiri kwamba kila kitu cha mwenzio ukijue. Sio sahihi lazima kuwe na uhuru wa kufanya mambo fulani, huwezi kutoa password za mitandao kwa mwenzako ili iweje, mambo ya kike anayochati mwanamke na wenzake unataka na wewe uwasome na ushiriki ili nini. Au mambo wanaume wanayoelezana wenyewe unataka na mkeo ayasome ili nini sasa. Kama mnapendana mtafanya kila kitu kama roho zenu zinavyowatuma na hakutakuwa na matatizo. Kuhusu mambo ya fedha, pia sio lazima kuelezana kiasi cha pesa kilichopo Bank, wala mtu hashurutishwi na si lazima ataamua mwenyewe kama kuna ulazima wa kufanya hivyo kwa ajili ya mipango ya maisha. Kwanza vitu unavyomkuta navyo mwenzako kabla ya ndoa, huna haki yoyote ya kuoji ila mtakavyochuma pamoja ndio mtu anakuwa na haki ya kuoji na kupangilia matumizi, hiyo ni kwa mujibu wa sheria. Kwa kifupi sioni ulazima wowote wa kupeana passwords za mitandao wala kuelezana kuhusu akiba kama kuna mapenzi ya kweli vinginevyo mapenzi hakuna ni kama kuchungana fulani kutokana na kutokuwa na uhakika wa mapenzi ya upande wa pili. Ukiona mtu anataka password na username zako na kuulizia salio lako la bank chunga sana huyo yuko kimaslai zaidi na sio mwaminifu kwa hiyo na yeye anafikiri na wewe uko kama yeye alivyo. Wezi wa mapenzi au mali yoyote huwa wanaogopa sana wao kuibiwa kwa hiyo huwa wanajihami sana, wote wenye maukuta ya fensi makubwa na walinzi kibao mara nyingi hao ndio wezi wakubwa na mafisadi wanaogopa sana wao kuibiwa.
 
si lazima kupeana pasword ya mitandao ya kijamii......

Ila kama accounts za benk na kadhalika ni vile atakavyojisikia kama unaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo, ila ni vema iwe baada ya ndoa, au miezi kadhaa baada ya ndoa

ila kabla hajampa password za atm nk amsome kwanza mkewe, maana baada ya ndoa ndo atakua 'real' sasa, na aangalie tabia ya mkeww, wanawake wengine ni 'majini wala fedha'........
 
Passwords..mh!
Ila kuhusu finances (it can b banking issues, shares and other investments)...they can discuss these na kupanga kama watafungua a joint account..if they share common investing fields then waamue kutokana na their income..they can discuss what other sources of income they can venture into etc..
ila ingependeza hivi wawe wameviongelea wakati wa uchumba...wakifunga ndoa ni kutekeleza..na actually vingine (like investing) wawe wameshaanza kufanya!
otherwise, wapeane uhuru na personal space (hata kama watadiscuss their finance) ni vyema kila mmoja awe na personal account ya kufanya yale ambayo anataka kufanya!!!
 
Sasa si wanakwenda kuwa mwili mmoja katika Kristu na wanaaminiana ndo maana wakafikia kuoana sasa pasword zao kwa nini iwe shida wakati wanapendana? Mi naona kusema ukweli maamuzi haya ni mazito lakini inatakiwa kwanza wasomane kiaina maybe baada ya kuoana ndo wawekane wazi hizo password otherwise kwa sasa it is too early no matter what
 
Swali ni: ILI NINI!?? utakuwa una log-in kwenye account yake ili?
vi2 vingine hata mkiwa mwili mmoja havileti mantiki bana!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom