Msaada kwa anayeijua vizuri Gairo ya Morogoro

Pendesha

Member
Joined
Apr 18, 2013
Posts
99
Reaction score
60
Jamani, nawasalimu kwanza. Naombeni mnisaidie kunipa picha halisi ya wilaya ya Gairo mkoani Morogoro. Kigeographia , kiuchumi pamoja na kisiasa. Asante.
 
Gairo ni wilaya mpya iliyojitenga kutoka wilaya Kilosa.
Kaskazini imepakana na wilaya ya Kilindi,Mashariki imepakana na Mvomero,Magharibi imepakana na Kongwa na kusini imepakana na Kilosa...
Kuna misimu miwili ya mvua mvua za vuli huanza Dec.hadi Febr..na mvua za masika huanza March-June..
Usafiri..wilaya hii imepitiwa na Barabara kuu ya Dar-Mwanza...
Mazao:Mahindi,Viazi vitamu,maharage,Alizeti
Hali ya hewa ni baridi kiasi mda wote...
Kabila dominant ni Wakaguru
Miji maarufu ni Gairo,Mtumbatu,Maguha,Berega,Chakwale
Nimekusaidia kidogo mkuu wangu
 
hapo kama anajua kusoma ataelewa tu
 
Jamani, nawasalimu kwanza. Naombeni mnisaidie kunipa picha halisi ya wilaya ya Gairo mkoani Morogoro. Kigeographia , kiuchumi pamoja na kisiasa. Asante.
Home Sweets Home Mkuu Pendesha Karibu Sana Mkuu,Najua itakuwa issue za transfers kikazi hizo au nimebugi??
 
Udongo wake mwekundu sana halafu maji ni shida sana! ila kama ulipitia mafunzo ya JKT utaishi vizuri tu lakini kama ni mtoto wa mama mhhhhh itakuwa soo!
 
Mbunge wa hapo ni ccm
Wakazi wake wanipenda sana ccm licha ya matatizo uliyosoma hapo juu

Usiache kuipigia kampeni ccm
 
Shukran sana wakuu wangu kwa msaada wenu bila shaka niliyo kuwa nayahitaji naona tayr mmenisaidia.
Sina mengi sana zaidi ya kusema undugu wetu ,mshikamano wetu,tukiwa wamoja hivi basi hakuna shida tena.
Kazi njema na Mungu awabariki.
 
Gairo ni wilaya mpya iliyojitenga kutoka wilaya Kilosa.
Kaskazini imepakana na wilaya ya Kilindi,Mashariki imepakana na Mvomero,Magharibi imepakana na Kongwa na kusini imepakana na Kilosa...
Kuna misimu miwili ya mvua mvua za vuli huanza Dec.hadi Febr..na mvua za masika huanza March-June..
Usafiri..wilaya hii imepitiwa na Barabara kuu ya Dar-Mwanza...
Mazao:Mahindi,Viazi vitamu,maharage,Alizeti
Hali ya hewa ni baridi kiasi mda wote...
Kabila dominant ni Wakaguru
Miji maarufu ni Gairo,Mtumbatu,Maguha,Berega,Chakwale
Nimekusaidia kidogo mkuu wangu

mkuu kula tano
 
zamani walikuwa wanatumia maji ya bomba toka milima ya karibu na kisitwi. Kwa sasa sijui.
 
Kama umehamishiwa pale umeumia. Usiku baridi mchana joto. Pale Chadema au Bavita hawana tawi. Kiujumla bora uhonge usipelekwe pale.
 
daaaah gairo noma maji wanachota wanakijiji kwa tarehe kila mwez mtu ana tarehe yake na kule hata kama hujui kikaguru utajua tu sababu had mtoto aliyezaliwa leo akilia analia kikaguru PIA BARID NDIO USISEME JUA LIKITOKA NI SHEREHE PIA KULE HAKUNA GHOROFA NI NYUMBA ZA KAWAIDA TU
 
Back
Top Bottom