Msaada: Kujaribu kilimo cha mbogamboga Rufiji

Msaada: Kujaribu kilimo cha mbogamboga Rufiji

makolola

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2014
Posts
765
Reaction score
290
Wadau nahitaji kwenda kujaribu kilimo cha nyanya chungu,vitunguu,bamia,nyanya kule rufiji(daraja la mkapa).
Naombeni ambaye ameshajaribu kulima huko atoe uzoefu ya mazao ya bustani yanayokubali sana huko na changamoto za kilimo huko.
 
wajasiria mali wengi hawalimi rufiji?
 
Mkuu Kama Unataka Kufanikiwa Weka Nia Na Juhudi Ya Dhati Kisha Nenda Kafanye Na Si Kujaribu. Ukisema Unaenda Kujaribu Changamoto Ndogo Tu Utakimbia Mashamba
 
We jamaa lets meetbtiweke mikakati nilishawai kufika huko kwabutafiti mdogo tu. Changamoto kubwa ni mafuriko na pili miuondombinu ya ya kufika hama kusafirisha mazao toka mashambani. Na sijakuta watu wanafanya commercial zaidi ya wenyeji asee. But maeneo yapo bei kwa hekali mabaka laki 5, Kukodisha shamba mbaka laki na 50 kwa mwaka. wenyeji waliambia pia mamba pia kuna muda wanasumbua asee nilipata shamba mita 10 toka mtoni upande wa kulia kama unakwenda Mtwara/Lindi na km kama 7 toka barabarani i was huko mwezi wa Tano Kufanya utafiti. Mtaji tatizo
 
Wadau nahitaji kwenda kujaribu kilimo cha nyanya chungu,vitunguu,bamia,nyanya kule rufiji(daraja la mkapa).
Naombeni ambaye ameshajaribu kulima huko atoe uzoefu ya mazao ya bustani yanayokubali sana huko na changamoto za kilimo huko.
vipi mkuu umefanikiwa?
 
nipo rufiji hapa lakini tatizo wa huku hawajafikira kabisa kilimo ,kwa utafiti niliofanya ni kwamba rufiji kuna joto sana kiasi kwamba mjasiriamali anatakiwa kutafuta soko ili kuepuka kuoza kwa kitunguu,pia mamba kandokando na mto kitu ambacho ni hatar kwa mjasiliamali pamoja na kwamba ardhi yake ni bikra ,yaaani inarutuba mpaka nachanganyikiwa
 
Back
Top Bottom