Msaada kuhusu VISA ya kwenda china Kibiashara

Jumax

Senior Member
Joined
Mar 4, 2017
Posts
117
Reaction score
229
Habari ndugu wanajamvi,


Binafsi ninaomba msaada kwa anaetambua jinsi au ni hatua gani rahisi, halali na za HARAKA kuweza kupata visa ya kwenda china kibiashara,
Napenda kutanguliza shukrani zangu za dhati kabisa kwenu, Ahsanteni.
 
Reactions: SDG
maana nimejaribu kutafuta humu jukwaani kwa bahati mbaya sijapa kuona uzi unaoelezea kwa kina suala hili
 
Mkuu haina shida sana. Nenda ubalozini. Sema changamoto huwa nikuwahi asubuhi ili upate huduma mapema coz jamaa mwisho wa kufanya kazi ni saa tano ( Kama nitakuwa na kumbukumbu sawa). Kuna mida huwa kunakuwa hakuna watu kabisa but kuna time itakulazimu ufike pale hata saa 10 alfajir ili kuwahi namba za mwanzo. Vinginevyo utafute mtu wa kukushikia namba ambaye utamlipa.
 
Asante sana mkuu na huwa inachukua muda gani mpaka kupata visa mkuu?
 
Asante sana mkuu na huwa inachukua muda gani mpaka kupata visa mkuu?
Biashara Gani hiyo ambayo una haraka hivyo isije kuwa umemeza mzigo unataka kuwahi usikupasukie tumboni kule wananyonga ohoooo
 
Mwakibete wachina wanataka wageni wengi waende kwao kununua bidhaa hawana masharti magumu ya kupata visa na pia kama kuna vitu hauna wanakuelekeza ili ukamilishe upewe Visa sio kama USA ukiwa huna sifa umefeli hawakupi tena...usimtumie mtu fanya kila kitu mwenyewe labda agent ambae anatambulika na ubalozi kwa ajili ya kutolea Visa wageni...
 
Msaada jamani , juu ya upatikanaji wa Visa kwenda China,
Passport ninayo tayali, barua ya mwaliko ninayo, vitu vingine ni vipi ili niweze omba Chinese Visa
 
Msaada jamani , juu ya upatikanaji wa Visa kwenda China,
Passport ninayo tayali, barua ya mwaliko ninayo, vitu vingine ni vipi ili niweze omba Chinese Visa
Bhas umemaliza. Ingia kwa website yao, jaza taarifa zako zote utapata tarehe ya kwenda ubalozini ukiwa na hiyo appointment fomu pamoja na application form ambayo iko signed.

Jamaa hawana mambo mengi, ndani ya siku 3 unapata Visa yako na kama ni express bhas siku inayofuata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…