Msaada kuhusu tiba ya "Migraine Headache"

Utotole

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,604
4,259
Hello wana Forum,

Ni imani yangu kwamba baadhi humu mnautambua ugonjwa huo tajwa. Sasa mimi nina ndugu yangu wa karibu ambaye anasumbuliwa na kichwa ambacho kila nikitafakari nazidi kupata hisia kwamba kinasababishwa na tatizo hilo.

Kwanza kabisa ni dalili ambazo hutangulia "headache episodes", ambazo ni pamoja na kuona vitu nusu nusu (aura). Pia, kichwa kikali hutokea na mara nyingi upande mmoja huathirika zaidi, na hapa napata hisia kuwa inaweza kuwa hemiplegic migraine. Wakati mwingine episodes huambatana na "numbness and paralysis" upande mmoja wa mwili.

Tatizo hili hujirudia kila baada ya muda fulani pasipo mpangilio wowote.

Kwa dalili hizo, nakuwa na kila sababu ya kuipa uzito theory yangu kuhusu aina ya kichwa hiki.

Hata hivyo, kila anapokwenda hospitali na kujaribu kuwaeleza madaktari juu ya tatizo hilo, akishataja tu kuwa tatizo linahusiana na "maumivu ya kichwa", haraka haraka anamuvuzishwa kwenda kitengo cha macho, na huko wanapima zaidi mambo ya vision sijui na nini tena huko na mwisho wa siku anaangukia kwenye kupewa au kubadili mawani.

Sasa wana taaluma naombeni ushauri wenu:
1. Je, ni kweli tatizo hili linahusiana kwa namna yoyote na matatizo ya macho kama inavyotokea akienda hospitali?
2. Je, mawani yana msaada kiasi gani kupunguza au kuondoa tatizo hilo?
3. Ni Njia gani tunaweza kutumia kuhakikisha huyu ndugu anapata ahueni ya tatizo hiolo ama kuondokana nalo kabisa? Natambua wengine hapa ni wataalam (MD na tiba asilia), na wengine ni wahanga wa tatizo hili (walipata kuugua, wanaugua au wanauguza)

Asanteni sana kwa michango yenu ya maana.
 
Mwambie ndugu yako ale Lozi aka Almond punje 12 kila anaposhikwa na maradhi ya kichwa aka (Migraine Headache) tatizo lake litakwisha akipona uje ulete mrejesho wako.

Almond kwa kutibu maradhi ya kichwa.jpg
 
Back
Top Bottom