Hawa jamaa wanatumia kanuni ya MTEJA MFALME kabla ya kupata huduma na ukipata huduma slogan inabadilika japo hawasemi na kuwa MTEJA ----, Hata mie niliwahi kununua umeme wa LUKU jamaa aliniambia nimnunulie kwa niaba process yote ikakamilika but no umeme nikaenda Voda wakasema nenda Tanesco na nikaenda Tanesco wakasema nenda Voda mbaya zaidi niliekuwa namnunulia nae ni mchungu kwenye hela nilipompa hiyo story akachukulia poa kwa kuwa ela alikuwa hajanipa nilichokuwa nafanya ni kununua alafu ananirejeshea (hapa ndio machungu yalipozidi)
Transaction za kidigitali ni nzuri ila kwa mazingira kama haya wanatufanya tuzidi kupenda kufanya mihamala ya face to face kwani walichotakiwa ni kuweka utaratibu wa nini cha kufanya endapo mihamala ya namna hiyo inaposhindwa kufanya kazi.
Nenda TCRA japokuwaTCRA nao sijui majukumu yao ni nini maana kwa issue kama hizi nadhani wao ndio wahusika kuhakikisha watumia huduma za simu wanahudiwa kikamilifu na mbaya zaidi sidhani kama wapo digitally kiasi kwamba ukipeleka shida yako hata kama upo kijijini through simu unahudiwa, wao wapo busy na kampeni ya kutotumia lugha chafu kwenye mitandao sasa sijui ubora wa utoaji huduma nani anasimamia