Surface pump/booster ndio hizo unazoona zinakaa juu maji yanakua chini.zinauwezo wa kusukuma maji umbali mrefu lakini si kunyonya.Hivo kama maji yako karibu kama maji ya ziwa,mto au kisima kifupi si zaidi ya mita saba. Zinafanya kazi vizuri.hizi ni pump ambazo zimefungwa na engine au motor na hazilowekwi ndani ya maji.
Submersible pump, hii ni maalum kwa visima virefu kuanzia mita nane kwenda chini.zina uwezo mzuri wa kupandisha maji kutoka chini Kuja juu. Total head. Hii unahesabu kutoka pump ilipo hadi kwenye tank vertical. Ni vizuri kutumia submersible pump kwa kisima maana hata maji yakipungua itasukuma inashauriwa uweke tank,ili ifanye kazi moja yaani kupandisha,na si kuipa na kazi ya pili kusafirisha hayo maji. Kwa ufupi ni hayo