Msaada kuhusu mtoto wa namna hii

Msaada kuhusu mtoto wa namna hii

Lugumgya

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2019
Posts
629
Reaction score
2,053
Miaka mitatu iliyopita, Mdogo wangu alimpachika mimba binti mmoja hivi.

Baada ya ile mimba kuingia, waliingia katika mgogoro Mkubwa Sana. Mgogoro wenyewe ulihusu kutokubaliana juu ya kuitoa au kutoitoa. Dago akitaka itoke na mdada akipinga jambo hilo. Baada ya kutofikia muafaka dogo alikata mawasiliano na jambo hilo lilikuwa lao peke yao. Mimba ilivyofikia miezi minne, binti aligundulika kwao kuwa ana ujauzito, na akafukuzwa kwao, ndipo alipofanya jitihada za kumtafuta tena dogo na wakakubaliana wakaitoe tu.

Kweli wakafanikiwa kukubaliana kwenda kuitoa ile mimba hospitalini. Walipofika hosipital Dr. akamfanyia vipimo mdada na baada ya kumfanyia vipimo akawaambia mtoto hana tatizo lolote tumboni hivyo nafsi yake imesita kufanya mauaji

Akawashauri Sana (kwa mujibu wa Mdogo wangu) akajitolea hadi kutoa msaada katika malezi ya ile mimba pale watakapohitaji msaada wake, baada ya kuwa wamempa Maelezo kwamba wanafanya hivo kutokana na kukosa uwezo wa kulea mimba hiyo, na baadae kumudu gharama za malezi na makuzi ya mtoto. Mbele ya Dkt. Wakaafikiana kutoitoa.

To cut the story short, mtoto alipozaliwa shemeji alikuwa anakaa kwa shangazi yetu. Mtoto alivyofikisha miezi mitatu yule binti alirudi kwao na mtoto. Amekaa huko, na mtoto hadi mwaka jana, mama ake akatoa taarifa kuwa anataka kurudi shule hivyo dogo achukue mtoto wake.

Baada ya kusikia Maelezo hayo, niliamua kujitolea kumchukua huyo mtoto. Mpka saiv nakaa naye lakini, visa Sasa;
1. Jambo unalomkataza ndo anafanya.
2. Akisema sitaki ana maanisha.
3. Anaweza kutaka kujisaidia akatoka na kwenda kujisaidia kitandani au kwenye makochi sebuleni mchana kweupe.
4. Niliamua kumpeleka baby school akacheze na wenzake, lakini anawang'ata wenzake balaa na kukojoa au kujisaidia Darasani kwa makusudi.
5. Kuna wakati anatishia nitachukua jiwe nivunje TV!

Visa ni vingi wadau. Kuna wakati nashindwa kuelewa kama kweli mtoto ni wetu, lakini kuna vitu tunafanana nae. Baba yake bado hajasettle kuweza kumhudumia.

@mshanajr na wengine! Ishu hapa ni nn? Na nimfanyej! Kule ukweni ndo hawatoi ushirikiano kabisaa!

Nawasilisha kwa ushauri.
 
Duh! Mkuu wewe ndo mlezi wake inabidi ufanye jitihada zote ajue kizuri na kibaya...naimani mtoto mdogo hawezi kukushinda ukiwa serious, usitegemee ushirikiano upande wa pili ilihali mtoto ni wenu..usisahau kusali.
 
Mtoto umleavyo ndio akuavyo,mtoto hujifunza vitu katika mazingira yanayomzunguka katika makuzi yake,

Angalia jinsi maisha yanavyokwenda hapo kwako,je mtoto ana copy toka kwa nani hizo tabia? Jaribu kumlea kwa misingi yenye maadili,ajue lipi baya na lipi zuri,kipi afanye muda gani na afanyie wapi? Huyo mtoto bado nimdogo hajajua lipi baya na lipi zuri,wewe na walio karibu nae hapo home ndio walimu wake,Bado hujachelewa mkuu,Achana na imani za kishirikina,hakuna uchawi hapo.
 
Ahsante Mkuu!
 
Huyo mtoto tayari anaroho ya kukataliwa ndani yake. Hivi wanaume mkoje lakini? Unakataaje mtoto ambae ametoka kiunoni mwako? Kama unaweza kuruhusu damu yako iuwawe hotoshindwa mchimja mtu live.

Sasa kwenye ulimwengu wa roho iko hivi; since the day huyo baba alikataa mimba hiyo isiishi, roho ya kukataliwa ilimwingia huyo innocent child (so sad), mtoto anaweza jikuta anatabia ambazo kila mtu atakataa kukaa naye. Anzia hapo kwa bibi mtu ashamkataa anataka nyie ndo mkae nae, wewe nawe unadalili za kurudisha mpira kwa kipa, and the cycle continues, hilo liroho la kukataliwa litampa huyo mtoto asiye na hatia tabia amabazo watu hawatapenda kukaa naye, watamkataa.

fanyeni hima mpate msaada wa kiroho kumuokoa huyo mtoto.
 
Huyo mtoto ana hasira na familia yenu maana mlitaka kumuua wakati yuko tumboni na hapo bado atawasumbua sana hadi anakua na mtakereka hadi mtaona bora tu mimba ingetolewa ndipo mtaposhangaa atapowaambia Mungu hakupenda yeye afe
 
Hebu mzungumzishe na mboko watoto wa kiafrika hawaendi kizungu..😅
 
Huyo mtoto tayari anaroho ya kukataliwa ndani yake. Hivi wanaume mkoje lakini? Unakataaje mtoto ambae ametoka kiunoni mwako? Kama unaweza kuruhusu damu yako iuwawe hotoshindwa mchimja mtu live.

Sasa kwenye ulimwengu wa roho iko hivi; since the day huyo baba alikataa mimba hiyo isiishi, roho ya kukataliwa ilimwingia huyo innocent child (so sad), mtoto anaweza jikuta anatabia ambazo kila mtu atakataa kukaa naye. Anzia hapo kwa bibi mtu ashamkataa anataka nyie ndo mkae nae, wewe nawe unadalili za kurudisha mpira kwa kipa, and the cycle continues, hilo liroho la kukataliwa litampa huyo mtoto asiye na hatia tabia amabazo watu hawatapenda kukaa naye, watamkataa.

fanyeni hima mpate msaada wa kiroho kumuokoa huyo mtoto.
Ahsante dada kwa ushauri mzuri. Sina lengo la kurejesha mpira kwa kipa, nahitaj tumsaidie mawazo yenu ni muhimu kwa Ustawi wake. Kama ulivyoshauri hivi. I then send you [emoji181]
 
Mkuu nimesomea saikolojia ya watoto kuna njia nyingi unaweza muwin mtoto.....kitu cha kukumbuka mtoto humsikiliza yule anaempenda, so jitahidi ujenge mazoea mtoto akupende na usipokuwepo akumiss na kukutaja kabisa

kuna njia nyingi unazoweza kutumia akakupenda tumia zawadi ndogondogo juice,pipi na vingine vitam unanunua unakaa nae chini anakula ukiwepo,.... pili kucheza nae me watoto nikikaa nao dakika 10 nyingi ataanza cheka na kunirukia rukia na kuomba tucheze (kukimbizana wanapenda sana au kumuonesha picha za vitu au kumchekesha)....

pia usiwe mkali sana na penda kuongea nae kwa wewe kukaa kwenye kiti au kuchuchumaa muwe sawa, unamuambia alafu unarudia kile kitu yeye akujibu, mfano unamwambia sio tabia nzuri kujisaidia kitandani watu hujisaidia chooni, umenielewa? Atasema ndiyo, unamwambia watu hujisaidia wapi? Atasema chooni....

Jitahidi usiongee nae ukiwa umesimama kaa chini au chuchumaa, onesha kumpenda angalia nae cartoon kwenye simu,mpe zawadi, mhug na kumwambia asante akukupa kitu,

Kwa watoto wadogo kuwa mkali haisaidii hata kidogo tumia njia ya upole na kujali atakuwa vizuri sana as time inasogea, pia maombi muhimu Mungu ampe mtoto utulivu ili urahisishe kujifunza hata akiwa shuleni.....
 
Amina Mkuu. Ahsante Sana. Nimekuelewa vizuri Sana. Nitajitahidi kurekebisha pale ninapohisi nimekwama kutokana na huu ushauri wako.
Hata inbox nitakuibukia kwa ajili ya nyongeza. Zaidi tumuokoe huyu mtoto.
Barikiwa Mkuu.
 
Asante mkuu nipo tayari kutoa msaada muda wote....Mungu akusimamie katika kipindi hiki kule sio kazi rahisi kabisa
 
Huyo mtoto tayari anaroho ya kukataliwa ndani yake. Hivi wanaume mkoje lakini? Unakataaje mtoto ambae ametoka kiunoni mwako? Kama unaweza kuruhusu damu yako iuwawe hotoshindwa mchimja mtu live.

Sasa kwenye ulimwengu wa roho iko hivi; since the day huyo baba alikataa mimba hiyo isiishi, roho ya kukataliwa ilimwingia huyo innocent child (so sad), mtoto anaweza jikuta anatabia ambazo kila mtu atakataa kukaa naye. Anzia hapo kwa bibi mtu ashamkataa anataka nyie ndo mkae nae, wewe nawe unadalili za kurudisha mpira kwa kipa, and the cycle continues, hilo liroho la kukataliwa litampa huyo mtoto asiye na hatia tabia amabazo watu hawatapenda kukaa naye, watamkataa.

fanyeni hima mpate msaada wa kiroho kumuokoa huyo mtoto.
Hapo tatizo ni kwa wote wawili. Usimlaumu mwanaume. Inavyoonekana hawakukaa na kujadiliana wakati wa kupata mtt.
Kwa maneno rahisi hiyo mimba imepatikana kwa suprise. Haikupangwa. Wazungu wana iita "Unwanted pregnancy"
Bahili nitatizo kubwa ktk jamii yetu.
Kitu inayoitwa huduma staha kwa wajawazito/ Wazazi (Respective maternity care) pamoja na ushiriki wa wanaume clinic ya uzazi (Male involvement) zinashinfikanika kutokana na mimba za aina hii yaani zisizopangwa.
Kwa hiyo ni muhimu wenza kujadiliana na kupanga uzazi ili mambo yaende sawa.
 
Hebu mzungumzishe na mboko watoto wa kiafrika hawaendi kizungu..[emoji28]

Mboko kweli zinasaidia ila hapa inaonesha kuna kitu cha ziada,kwa watu wa imani kuna kitu kimeongelewa roho ya kukataliwa,ni kitu kibaya sana tena sana.
 
Huyo mtoto tayari anaroho ya kukataliwa ndani yake. Hivi wanaume mkoje lakini? Unakataaje mtoto ambae ametoka kiunoni mwako? Kama unaweza kuruhusu damu yako iuwawe hotoshindwa mchimja mtu live.

Sasa kwenye ulimwengu wa roho iko hivi; since the day huyo baba alikataa mimba hiyo isiishi, roho ya kukataliwa ilimwingia huyo innocent child (so sad), mtoto anaweza jikuta anatabia ambazo kila mtu atakataa kukaa naye. Anzia hapo kwa bibi mtu ashamkataa anataka nyie ndo mkae nae, wewe nawe unadalili za kurudisha mpira kwa kipa, and the cycle continues, hilo liroho la kukataliwa litampa huyo mtoto asiye na hatia tabia amabazo watu hawatapenda kukaa naye, watamkataa.

fanyeni hima mpate msaada wa kiroho kumuokoa huyo mtoto.
Hizo ni tabia tu za mtoto,atabadilika mybi kuna upendo anakosa
 
Unajua mkuu hata mi nlikuwaga hivo nlikula mboko kwa Maza mpaka nikatulia jaribu kuwa mkali kwake Yani unakuwa mkali kwelikweli hutojuta daima
 
Hawa kina Diamond na mabifu yao na wazee wao.huwa tunayachukulia poa sana na kumuona Diamond kama hajitambui.. kumbe huenda wana siri.nzito sana hawa.. ukute wazee wao.walishajaribu kuwaua walipokuwa tumboni ikashindikana wakawasusa.. KARMA!!
 
Miaka mitatu iliyopita, Mdogo wangu alimpachika mimba binti mmoja hivi.

Baada ya ile mimba kuingia, waliingia katika mgogoro Mkubwa Sana. Mgogoro wenyewe ulihusu kutokubaliana juu ya kuitoa au kutoitoa. Dago akitaka itoke na mdada akipinga jambo hilo. Baada ya kutofikia muafaka dogo alikata mawasiliano na jambo hilo lilikuwa lao peke yao. Mimba ilivyofikia miezi minne, binti aligundulika kwao kuwa ana ujauzito, na akafukuzwa kwao, ndipo alipofanya jitihada za kumtafuta tena dogo na wakakubaliana wakaitoe tu.

Kweli wakafanikiwa kukubaliana kwenda kuitoa ile mimba hospitalini. Walipofika hosipital Dr. akamfanyia vipimo mdada na baada ya kumfanyia vipimo akawaambia mtoto hana tatizo lolote tumboni hivyo nafsi yake imesita kufanya mauaji

Akawashauri Sana (kwa mujibu wa Mdogo wangu) akajitolea hadi kutoa msaada katika malezi ya ile mimba pale watakapohitaji msaada wake, baada ya kuwa wamempa Maelezo kwamba wanafanya hivo kutokana na kukosa uwezo wa kulea mimba hiyo, na baadae kumudu gharama za malezi na makuzi ya mtoto. Mbele ya Dkt. Wakaafikiana kutoitoa.

To cut the story short, mtoto alipozaliwa shemeji alikuwa anakaa kwa shangazi yetu. Mtoto alivyofikisha miezi mitatu yule binti alirudi kwao na mtoto. Amekaa huko, na mtoto hadi mwaka jana, mama ake akatoa taarifa kuwa anataka kurudi shule hivyo dogo achukue mtoto wake.

Baada ya kusikia Maelezo hayo, niliamua kujitolea kumchukua huyo mtoto. Mpka saiv nakaa naye lakini, visa Sasa;
1. Jambo unalomkataza ndo anafanya.
2. Akisema sitaki ana maanisha.
3. Anaweza kutaka kujisaidia akatoka na kwenda kujisaidia kitandani au kwenye makochi sebuleni mchana kweupe.
4. Niliamua kumpeleka baby school akacheze na wenzake, lakini anawang'ata wenzake balaa na kukojoa au kujisaidia Darasani kwa makusudi.
5. Kuna wakati anatishia nitachukua jiwe nivunje TV!

Visa ni vingi wadau. Kuna wakati nashindwa kuelewa kama kweli mtoto ni wetu, lakini kuna vitu tunafanana nae. Baba yake bado hajasettle kuweza kumhudumia.

@mshanajr na wengine! Ishu hapa ni nn? Na nimfanyej! Kule ukweni ndo hawatoi ushirikiano kabisaa!

Nawasilisha kwa ushauri.

Halafu na wewe unataka mtoto wa miaka miwili.awe na akili.na busara kama mtu mzima? ..hapo ni sawa na kwenda kumshitaki mahakamani mtoto wa miaka miwili .

lazima hakimu na wazee wa mahakama washikwe na butwaa
 
Back
Top Bottom