Msaada kuhusu mkopo wa chuo

Msaada kuhusu mkopo wa chuo

amina ngalo

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2013
Posts
309
Reaction score
170
Ndugu wanaJF,

Naombeni msaada,

Kuna mtoto wa shemeji yangu ni yatima, suala lake la mkopo halieleweki kama upo au haupo, amepangwa chuo cha St. Agustino huko Dodoma.

Mpaka sasa haijulikani kama anapata mkopo au hapati, yupo Dar kwasasa amefuatilia hayo mambo ya chuo.

Msaada ninaoutaka ninamna ya kumsaidia apate mkopo, pili hivi yatima hawana kipaumbele kwenye hii mikopo?

Mwenye mawasiliano na TCU naomba.
 
Magufuli kasema hivyo vyuo vya St ...nani sijui havina hadhi ya kuwa vyuo vikuu vitageuzwa VETA.
 
Mkuu hicho ni st. Jon not st. Augustne , hicho kpo mwanz
 
mkopo una vigezo, huyo ndg yako kasoma masomo gn
 
Hii Id itakuwa iko hacked. Amina Ngalo nimjuae mimi ni mtu wa kutetea kila upuuzi wa CCM na ni miongoni mwa misukule ya Lumumba iliyobaki pale Arusha. Wewe uliyepost uzi huu itakuwa ni mwizi wa akaunti za wengine.
 
Pole ndug
ndugu wanajf naombeni msaada kuna mtoto wa shemeji yangu ni yatima suala lake la mkopo halieleweki kama upo au haupo amepangwa chuo cha st Agustino huko Dom.

mpaka sasa haijulikani kama anapata mkopo au hapati yupo Dar kwasasa amefuatilia hayo mambo ya chuo

msaada ninao utaka ninamna ya kumsaidia apate mkopo .pili hivi yatima hawana kipaumbele kwenye hii mikopo ??
mwenye mawasiliano na TCU naomba

Pole ndugu.Hii inatufanya sisi kama watanzania kuanza kufikiria mbinu mpya (ideas) za kusaidia watu kama hawa.Ni lazima nchi igeuze utaratibu wake katika mambo mengi ikiwa ni pamoja na jambo kama hili linalowakilisha mamia ya YATIMA na any DISADVANTAGED people!

Nchi nyingi zina mfumo huu unsoitwa MFUKO WA FADHILI -BURSARY FUND kwa wasio na Uwezo.
Je Tanzania TUNAO?
Ukienda Africa ya Kusini kuna SAMA- South African Medical Association. Inasomesha wale wasio na UWEZO LAKINI iwe tu katika FANI ya UDAKTARI.
Hata Zimbabwe na Swaziland na nchi nyingi za kiafrika na hata baadhi ya jirani zetu na nchi nyingine mpaka Marekani zina mambo kama haya.

MFUKO huu unaweza kuwa wa KISERIKALI ambapo PESA kiasi millioni kadhaa zinapelekwa katika kila WILAYA ama...na kusimamiwa.Na WABUNGE na VIONGOZI wengine kama vile wenyekiti wa Kamati ya ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na VIONGOZI wa DINI. Wanapitia kila ombi ili KUJUA USTAHILI wa mwombaji.

Hapo ndipo fedha zinatolewa analipiwa CHUO Je ni lini tutakuwa na mawazo kama hayo ya YATIMA enyi viongozi wetu?
 
St Augustine kipo mwanza(headquarter),tabora,kagera,mtwara.Dodoma sidhani,itakua St John.
 
Back
Top Bottom