Msaada kuhusu kuagiza gari nje ya nchi (Japan)

kakamgeni

JF-Expert Member
Feb 1, 2018
241
201
Mambo vipi wadau wa jukwaa hili, bila shaka kuuliza sio ujinga, mara kwa mara nimekuwa nikipita kwenye website za kuuza magari hasa za Japan kama vile "Be Foward" na "SBT".

Nimekuwa nikiona jinsi walivyojipanga vizuri kuanzia suala zima la uaminifu katika biashara ya kuuza magari na vipuri vyake, kwa hili nawapa pongezi za dhati kabisa.

Swali langu ni kama ifuatavyo; Unakuta umechagua gari mfano Vitz, uzuri wanakuwekea na gharama za gari na usafirisha mpaka katika bandari iliyo karibu mfano hapa Dar ni TPA, hiyo wanaita CIF: Cost, Insurance & Freight, halafu baada ya hapo ipo link wameweka ya TRA Calculator kwa ajili ya Customs Tax (Kodi).

Mfano kwa gari niliyochagua CIF = Tsh 4,735,256 na Customs Tax = 3,710,222 ambapo kwa jumla yake unapata Tsh 8,445,4778/= bila chenji.

Sasa hapa kinachonitatiza ni kwamba huwa nasikia wakati mwingine gharama hii huenda ikazidi na endapo usipokuwa na emergence fund basi gari uliyoagiza huenda ikapigwa mnada.

Hilo la kwanza, la pili ningependa kufahamu taratibu zinazotakiwa kufuatwa kabla na baada ya gari kufika hadi kutolewa nje ya bandari kwa ajili ya matumizi binafsi na je, naweza kuagiza gari mwenyewe na kulitoa mwenyewe bila msaada wa watu wa clearing & forwarding?

Nawasilisha.
 
Ingia www.tra.go.tz
**Ukiagiza uwe na Subra! Wiki 6/7!toka Gari kupakiwa Japan pia uwe na hela ya akiba calculator ya TRA usiiamini sana unaweza kuacha Gari bandarini! Wadau wakalipiga mnada kwa Tsh. 18,500/=.
 
Back
Top Bottom