Msaada kuhusu Kipandikizi

supercharger GT

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
1,012
1,955
Habari zenu wakuu? Naona bado tupo Januari bhana! Ndugu zangu hili nalotaka kuuliza sijajua kama ni sehemu yake sahihi humu au vipi japokua linahusu mahusiano kiasi fulani!

Nina rafiki yangu wa muda tu tunafanya naye kazi Ofisi moja, sasa leo kaniuliza jambo kama ushauri kwa kwel namimi limenishinda nikaona nilete humu kwa kulijua mimi pia!

Ni hivi ana girlfriend wake wa muda mrefu, wamekuwa wakitumia condom sana, ila ikafika mahali wakaanza kwenda peku baada ya kuzoeana, sasa mdada akadaka mimba kimya kimya akatoa maana anajua jamaa asingekubali kutoa kwa wakati ule(ingawa mshkaji alisanuka ila akakausha tu).

Sasa bibie akaja na kinga mpya akamshauri jamaa amruhusu akaweke kipandikizi, njia mojawapo ya uzazi wa mpango. Sasa jamaa anachonieleza ni kuwa wamekiweka tangu mwaka jana mwezi wa 6 hivi, kipindi hcho hakikuwa na tatizo lolote , ila mambo yamechange kuanzia December hivi kwamba mdada anaweza pata period ikapitiliza ikaenda hata siku 10 au zaidi wakati kawaida alikuwa anaenda siku tatu zikizidi sana ni tano!

Jamaa anapata wasiwasi kuwa huenda ni kile kidude ndo kinasababisha au ni suala lile la kutoa mimba enzi zile??? Mwenye uelewa na hii kitu pia akinielezea na madhara ya Uzazi wa Mpango itakuwa poa! Asanteni wakuu
 
Aende akamuone mtoa Huduma nasemea hivyo nikiwa na maana kuwa hizi njia za uzazi wa mpango huwa zinakuwa na maudhi madogo madogo na ni vitu vya mda tu,kwahiyo ni vizuri kwenda kwa mtoa Huduma ili aweze kusaidiwa.
Nashukuru
 
Wala asiwaze aende kituo chair afya akainane na wataalamu wa family planing. Hayo hua ni maudhi madogomadogo na hutokea miezi mitatu ya mwanzo ila kwa ushauri zaidi aende akapate Huduma ..Asante
 
Back
Top Bottom