Baba Watoto
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 393
- 278
Wanajamvi habari za wakati huu,
Baada ya purukushani za kama miaka miwili hivi baada ya kujaza fomu ya kuomba kuunganishiwa huduma ya maji katika kibanda changu maeneo ya kibamba, (muda mrefu ni uzembe wangu kwa kuwa mama watoto alinisaidia kuficha fomu ikawa haionekani).
Hili tangazo la maji kuunanishwa kwa laki mbili lilifufua matumaini yangu kuwa na mimi nitakua na maji mjengoni basi nikabeba fomu yangu na kwenda ofisi zao, kwanza nikaambiwa ile haifai tena nijaze upya fomu, kwa kutumia technical know-who nikafanikiwa kuondoka na mafundi wao kwenda kufanya survey ambapo zilipatikana mita 270 toka bomba la kuunganishia, sasa maajabu ni hiyo bei niliyoambiwa kuwa natakiwa nitoe milioni mbili ili maji yaweze kuwepo hapo mjengoni.
Nikahoji vipi kuhusu laki mbili? Jibu ni kwamba laki mbili nikwa wateja wale walioko mita 20 toka bomba lilipo, na kwamba hapo kwangu gharama ya vifaa peke yake ni kama TZS 1.6 M, nina wasiwasi na makadirio haya kama kuna mtu anajua jinsi wanavyofanya au ameunganisha maji hivi karibuni.
Wakati huo huo naanza kufikiria kuchimba kisima aseee.
Nawasilisha.