Msaada kuhusu chuo cha Archbishop James University (AJUCO)-Songea

NGOSWE2

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
1,424
Reaction score
1,713
Nina kijana wangu kamaliza kidato cha sita mwaka huu, sasa kuna rafiki zake wanamchanganya kuhusu chuo. Kila mara anaongelea kuhusu Archbishop James University (AJUCO) kilichopo Songea, na imekuwa kero kwangu sana. Naomba anayekijua chuo hiki kwa habari ya ubora wa taaluma. Hasa kwa upande wa sayansi.
 
Anataka akasome nn huko AJUCO....!?? Afu Ki-gugo kwa msaada zaidi mkuu
 
Kama anajielewa mpe uhuru Mkuu, Ila kama unaona bado hajakomaa kuwa na msimamo umchagulie wewe(Ila uwe na uhakika na chuo unachompeleka)
 
Ni kweli mkuu kama ulivyosema. Kuna baadhi ya vyuo ambavyo mimi ninavifahamu. Lakini kelele za huyu kijana zimenifanya niombe ushauri kwa wadau wengine wanaweza kuwa wanakijua hiki chuo pia ili kama kina ubora nimkubalie.
 
hiki chuo mii nakijua na kuna best angu yupo pale anachukua md first year, alisoma cbg alipata 1 ya 7,, ni chuo kizur hakina competion sana kwa md,, kipo nnje kdg ya songea kwa kozi za md, kwa edction kpo toun pale pale,,,
 
Nina kijana wangu kamaliza kidato cha sita mwaka huu, sasa kuna rafiki zake wanamchanganya kuhusu chuo. Kila mara anaongelea kuhusu Archbishop James University (AJUCO) kilichopo Songea, na imekuwa kero kwangu sana. Naomba anayekijua chuo hiki kwa habari ya ubora wa taaluma. Hasa kwa upande wa sayansi.
 
Attachments

  • Screenshot_20170701-001344.png
    Screenshot_20170701-001344.png
    126.4 KB · Views: 89
Mikijana wangu aliwahi kuniletea mambo ya marafiki....
Nilichokifanya nilimpa makonde ya haja, alafu nikapiga kimya kama wiki moja hivi.... No salam. Mwisho nilimuambia akitaka tuende sawa, anapaswa tukae mezani Mimi na yeye na kisha anieleze kila anacho kihitaji na lazima anipe sababu (ushawishi).
Baada ya hapo tulielewana mimi na yeye, na nikamwambia sitaki habari za marafiki
 
hiki chuo mii nakijua na kuna best angu yupo pale anachukua md first year, alisoma cbg alipata 1 ya 7,, ni chuo kizur hakina competion sana kwa md,, kipo nnje kdg ya songea kwa kozi za md, kwa edction kpo toun pale pale,,,
Asante mkuu
 
Mikijana wangu aliwahi kuniletea mambo ya marafiki....
Nilichokifanya nilimpa makonde ya haja, alafu nikapiga kimya kama wiki moja hivi.... No salam. Mwisho nilimuambia akitaka tuende sawa, anapaswa tukae mezani Mimi na yeye na kisha anieleze kila anacho kihitaji na lazima anipe sababu (ushawishi).
Baada ya hapo tulielewana mimi na yeye, na nikamwambia sitaki habari za marafiki
Kiongozi kama umeniona vile! Jana tu ametoka kupewa mkong'oto. Yaani alitaka yeye ndio awe baba ndani ya nyumba. Lakini baada ya hasira kutulia na ndipo nikaomba ushauri japo kuwa yeye hajui kinachoendelea.
 
Ipo siku atakuja kukuangusha mbele za watu,kuna dogo alikuwa anapigana na baba ake.
 
Ana bahati mbaya amezaliwa na mimi, maana moto wake anajua vema. Nami sipendi hata kidogo kupiga watoto. Huyu nafikiri huko boarding alikokuwa ndio kumempa ujeuri. Nami nimeona nimpashe mara ya mwisho ajue bado sijazeeka akasimulie huko chuoni anakotaka kwenda mkuu. Asijifanye baba kwenye nyumba yangu.
 
Mkuu,

Hiyo ni dhana na tatizo kubwa sana kwa vijana wetu. Punde tu baada ya kumaliza elimu yao ya Sekondari ya Juu, huwaza zaidi kuhusu kujiunga na Chuo. Hujidanganya na kuokoteza Uongo wa hapa na pale. Uongo huo na ushauri wanaopeana, hujijaza ujinga na uzandiki.

Yaani, kila Mara wao huwaza tu kuhusu kujiunga Chuo hata kabla ya matokeo kutoka. Sikatai wao kujishauri, La hasha!. Lakini, kujijaza ujinga ni aina mbaya ya tabia.

Cha msingi kaa naye chini, tafuta details za kutosha kuhusu Chuo husika. Muambie kwa nini anadhani Chuo hicho ni kizuri?
Muambie katika maelezo yake ajikite zaidi katika maeneo haya;
1) Mazingira ya Chuo
2) Ubora wa vifaa na walimu
3) Ushindani wa wataalamu wao baada ya kuhitimu.

Nakuhakikishia hana lolote analolijua. Wanadanganya tu kwenye magroup yako ya WhatsApp.

Unaweza kufatilia kuhusu hicho Chuo huku mitandaoni.
 
Asante mkuu! Hawa watoto wa miaka hii!!
 
Pole sana mkuu
Mara nyingi vyuo vya private vipo kibiashara zaidi na ndio maana unaona promotion. Sababu system ya udahili imebadilishwa kila chuo cha private kinatumia mbinu kuvutia wateja hususani kwenye magazeti

Kinachotakiwa mtulize huyo kijana wako mwambie asubiri matokeo ndio process zingine ziendelee

Akifaulu vizur omba Udsm, Muhammad, udom, kcmc na bugando vyote medicine na course zingine za afya
 
Asante mkuu kwa ushauri wako.
 
Mzee,

Nikupongeze.

Maana sio kazi rahisi, changamoto ni nyingi mno ambazo naamini umekumbana nazo hadi kijana kumaliza shule.

Pia nimpongeze na kijana pia kwa kuhitimu!

Kuhusu kichapo,

Basi usimtandike tena, ataathirika kisaikolojia, na pia ataweka chuki na wewe.

Naomba ujaribu kukaa nae, uongee nae kama rafiki sasa

Umuulize kwanini anahitaji kwenda hicho chuo.?!

Akikupa sababu zake, nawe umueleweshe kwanini unakipinga na umwambie chuo ambacho unahitaji aende, umpe na sababu zako!

Naamini atakuelewa na atakwenda kwa moyo mmoja.

Ninaongea haya nikiwa kama kijana chini ya miaka 25
 
AJUCO ni college ya St. Augustine University of Tanzania. Ni kweli wanatoa MD. Mwaka wa jana baraza la elimu ya udakitari Africa Mashariki na TCU walifungia vyuo kama vinne ambavyo havikukidhi vigezo wa kutoa elimu hiyo. Vyuo vya private na serikali vilikumbwa na kadhia hiyo lakini AJUCO HAIKUKUMBWA NA KADHIA HIYO.

Kwangu mimi naisoma hiyo kama chuo kilichokubalika na serikali. CUHAS Bugando ndio college ya kwanza SAUT kutoa medicine na sasa ni chuo kamili. Kutokana na ushindani uliopo ni vizuri kijana awe na option za kutosha pamoja na hii.

Mimi naamini wakati wa kufikiria vyuo ndo huu kwa kuangalia scenario zote za matokeo na kujua vyuo kama mnavyofanya sasa majibu yakitoka ni rahisi kujipanga. All the best.
 
Ni kweli mkuu kama ulivyosema. Kuna baadhi ya vyuo ambavyo mimi ninavifahamu. Lakini kelele za huyu kijana zimenifanya niombe ushauri kwa wadau wengine wanaweza kuwa wanakijua hiki chuo pia ili kama kina ubora nimkubalie.
Ulicho fanya ndio sahihi huu ni wakati mgumu kwa wazazi wengi. Watoto wana group _thinking. Issue kubwa itakuwa kuoanisha ufaulu wake na uchaguzi wake. Ushindani wa kuingia AJUCO si mkubwa kama ule wa MUHAS na vijana wengi last year walikosa nafasi za kusomea MD. Kama utapata mtu anaekifahamu uzungumze nae itasaidia zaidi lakini always kuna element ya risk kwenye mambo haya.
 
Back
Top Bottom