Msaada kuhusu android development

isyesye

Member
Joined
Aug 14, 2016
Posts
51
Reaction score
22
Wakuu msaada kwa mwenye ujuzi kuhusu huo uzi hapo..juuu.na wapi naweza jifunza online..
 
Wakuu msaada kwa mwenye ujuzi kuhusu huo uzi hapo..juuu.na wapi naweza jifunza online..
Inategemeana na kama uko tayari kulipa ama la. kama unataka bure inabidi ukomae na Youtube na tutorials za online mpaka uelewe. Kuna faida na hasara za approach hii.

1. Haulipi hata senti zaidi ya bundle lako la data
2. Unakutana na aina mbalimbali za walimu na masomo

Lakini pia kuna hasara zake.
1. Hakuna wa kumwuliza swali moja kwa moja ikiwa hukuelewa mahali. Most of the time waalimu hawa huruhusu comments na wakati mwingine inachukua muda kujibu kwa kuwa hufanya kama hobby na ktk extra time.
2. Unaweza kuwa overwhelmed au hata confused unapotafuta tutorials. Zingine ziko outdated na kama ndio unaanza hutajua ipi ndio ipi.

3. Vitu vingi itabidi ujifunze mwenyewe na kama code ikigoma kwa mfano, ku compile, hakuna namna ya kupata msaada wa haraka. Sehemu za kuuliza kama StackOverflow, et al zinahitaji at least ujue namna ya kutuma vitu huko (wana high standard na kwa beginner swali laweza kuwa locked/downvoted na kukuacha na frustration bila msaada).

Ukiamua kulipia ni kinyume cha kutolipia. Hasara za huyu zinakuwa faida na vice versa.

Kama uko tayari kulipia live courses kuna sehemu nyingi duniani kujifunza. Tunatarajia kuendesha kozi kwa ajili ya Java na kisha Android Development. Unaweza check hilo tangazo au check na website kwa details za kozi husika

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…