Hivi kama ule utaratibu uliopendekezwa na Mwigulu kwamba watu wote kuanzia miaka 18 na kuendelea wawe na tin namba ili wakatwe kodi kwa kila muhamala wanaoufanya, je ndio kusema ukipeleka hela benki kama umeuza mali yako fulani ndio unakatwa kodi juu kwa juu? Maana kuna baadhi ya benki ukiingiza hela nyingi lazima wakuhoji umezipata wapi.