Msaada: Kubadili Betri ya gari kutoka N40 Kwenda N50

Mwenda_Pole

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
281
66
Heshima mbele wadau
Nina gari dogo aina ya toyota corolla kama inavyoonekana kwenye hii picha
Screenshot from 2016-05-30 15:15:18.png

Hivi karibu imekua na tatizo la kuwaka kwani betri yake imeisha. Sijawahi kubadili betri tangu ninunue gari June 2012. Nimeshauriwa nibadili betri na kwa mujibu wa wadau natakiwa ninunue betri kubwa ya hiyo ninayotumia. Kwa sasa ipo Betri ya ukubwa wa N40 ila wadau wanasema nikinunua basi ninunue N50.

Swali: Je kuna madhara yeyote kununua betri ya size ya juu kulinganisha na size iliyokuja na gari?
Je, ni betri gani nzuri kwa gari ya size hii?
Gharama ya betri mpya inaweza kuwa tsh ngapi? duka gani?
Natanguliza shukrani
 
Mkuu ww badilisha haina tatizo Na mara nyingi sana watu hubadili hiyo kwa sababu Gari ikiwa inamizunguko mikubwa sana km Tax Na mengineyo Ni Nzuri km Ni mtu wa mishemishe km huna mizunguko mingi haina shida kubadilisha
 
Binafsi kubadili sioni kama kuna tatizo zaidi ya haya
1. Physical size... Gari ndogo mara nyingi sehemu inayokaa betri huwa na ukubwa sawa na betri iliyokuja na gadi. Ampare hour (Ah) Capacity (N40 = 40Ah, N50 = 50Ah) huendana na physical dimensions za betri. Kama unapotoa hiyo N40 panatosha kuweka N50, weka
2. Charging time ya betri inategemea na Ah capacity.... keeping all other factors constant, N40 itajaa kwa muda mfupi kuliko N50.

NB: huyo aliyesema utaharibu stator sidhani kama kuna technical reason yoyote zaidi ya imani tu...
 
Asanteh sana mkuu kwa ufafanuzi wako
 
Back
Top Bottom