Msaada Kesi ya Mirathi

abbas

Member
Apr 23, 2010
5
0
Baba yetu amefariki miaka 2 ililiyopita. Kabla ya kifo chake mwaka 1998 alioa mke mwingine na akaishi nae katika nyumba alipokuwa unaishi mama na wadogo zangu.

Mama akalalamika baba na mke wake mdogo wakampiga mpaka akapoteza fahamu na kumdhuru sana mwili. Lakini kwa ufupi mama akamushitaki mahakama ya mwanzo akidai nyumba yake na shamba ili kuwahudumia watoto wake 11 waliozaa pamoja ndani ya miaka ya zaidi ya 40 katika ndoa yake.

Mama alishinda hiyo kesi lakini bahati mbaya haki yake hiyo hakukabidhiwa kisheria. Baba na kaka yetu mkubwa wa mama mwingine alishirikiana kumfukuza mama katika nyumba yake maana wanapesa nyingi sana...ni matajiri wakubwa.

Alipofariki baba nikafungua kesi ya miradhi nikakubaliwa kuwa msimamizi. Lakini kabla ya kuanza kuzitafuta mali za marehemu mama alirudi mahakamani kuomba kabla ya kuzigawa mali za marehemu aliomba mahakama apewe kwanza mali yake aliyoipata katika ndoa yao. Mimi ombi hili nilikubaliana na ombi lake.

Mh hakimu akaandika kukazia hukumu ili mama apate share yake. Aliambiwa apeleke maombi yake kwa hakimu mkazi wa wilaya. Ombi lake kwa hakimu mkazi alikataa akidai suala hilo analifahamu huwezi kuruhusu mama apewe hizo mali maana hukumu haijataja ni mali gani alishinda katika hukumu hiyo. Akasema turudi tugawe mirathi.

Nikahisi kaka yetu mkubwa ambae anadai mali hizo ni zake amepitisha pesa tayari. Kwa kuwa sisi ni masikini tukakaa chini tena kutafakari cha kufanya.
 
Haki Mbinguni Duniani mabavu. Mtakuja mkatwe panga ukute nyumba yenyewe hata thamani yake haizidi milioni tano... Ushauri ninaokupa tafuta milioni mbili tatu umengee mama ako vyumba viwili apate pa kuishi. Wakati wenzake wanachuma mali yeye alikuwa bize kuzaa watoto kumi na moja ambao hawana msaada. Mama ako naye akili zake mbili... Sorry for that. Hii sio Dunia ya kurundika mitoto... Zaa watoto wachache utumie ujana wako kutafuta mali. Sasa baba ako kamzalisha watoto kumi na moja, kamzeesha kamuona hana maana kaenda kuchukua binti kigori na mirathi kamuachia...
 
Nimeandika thread inayofuta. Ila samahani jf ndo nimeitumia leo hope nitaprove inshallah[/Q

Baada ya kukaa chini na dada yangu tukashauria kutafuta mwanasheria ili atusaidie. Nilipata ushauri kwa mtu akaniambia niende ofisi za WLAC Dar watanisaidia. Nilipowaeleza wakasema wanayo ofisi ktk wilaya ya muleba nikapewa namba zao mama na dada wakazitafuta ofisi za WLAC na kuonana na mwanasheria jina nalihifadhi. Akaandika barua kwenda kwa hakimu mahakama ya mwanzo. Mama akarudi mahakamani hapo akampa hakimu barua hiyo copy zote za kesi ninazo. Pale alikutana na hakimu mpya akamuamulisha karani aandike kukazia hukumu ya mali azoshinda wakati wa uhai wa baba. Karani wakadai hilo suala hakimu wa wilaya alilikataa hivyo mama arudi tena wilayani. Baada ya mzungu huo wakarudi tena WLAC kumpa taarifa..yeye akadai ataongea na hakimu wa wilaya maana anazo kesi zake nyingine. Baada ya kuzidi kumuulizia huyo afisa wa WLAC Muleba akasema hakimu amekubali kutusaidia katika hii kesi. Tukamuuliza hakimu huyo alikataa ombi letu mwanzoni je ni kwa vipi ataweza kutusaidia wakati alisema hukumu haijataja mali azoshinda mama katika kesi yake ya madai na baba. Ila katika hukumu ilitaja shamba 2 na nyumba ya kuishi ambapo mama aliamuliwa kujenga nyumba nyingine na kufanya hivyo ila hiyo nyumba ya familia ya mama kaka amewapangisha watu.na mama anaishi mitaani tangia mwaka 2006. Naomba msaada nifanyeje maana nahisi afisa wa WLAC na nguvu alizonazo kaka nahisi kuna kitu. Asante sana ...atakayeona tuwasiliane private nipo tayari.
 
Haki Mbinguni Duniani mabavu. Mtakuja mkatwe panga ukute nyumba yenyewe hata thamani yake haizidi milioni tano... Ushauri ninaokupa tafuta milioni mbili tatu umengee mama ako vyumba viwili apate pa kuishi. Wakati wenzake wanachuma mali yeye alikuwa bize kuzaa watoto kumi na moja ambao hawana msaada. Mama ako naye akili zake mbili... Sorry for that. Hii sio Dunia ya kurundika mitoto... Zaa watoto wachache utumie ujana wako kutafuta mali. Sasa baba ako kamzalisha watoto kumi na moja, kamzeesha kamuona hana maana kaenda kuchukua binti kigori na mirathi kamuachia...
Asante sana...lkn sio kila suala lazima ujibu bora ukae kimya ....Nichumu busara za kukaa kimya ni bora kwa afya ya ubungo wako
 
Baada ya kukaa chini na dada yangu tukashauria kutafuta mwanasheria ili atusaidie. Nilipata ushauri kwa mtu akaniambia niende ofisi za WLAC Dar watanisaidia. Nilipowaeleza wakasema wanayo ofisi ktk wilaya ya muleba nikapewa namba zao mama na dada wakazitafuta ofisi za WLAC na kuonana na mwanasheria jina nalihifadhi. Akaandika barua kwenda kwa hakimu mahakama ya mwanzo. Mama akarudi mahakamani hapo akampa hakimu barua hiyo copy zote za kesi ninazo. Pale alikutana na hakimu mpya akamuamulisha karani aandike kukazia hukumu ya mali azoshinda wakati wa uhai wa baba. Karani wakadai hilo suala hakimu wa wilaya alilikataa hivyo mama arudi tena wilayani. Baada ya mzungu huo wakarudi tena WLAC kumpa taarifa..yeye akadai ataongea na hakimu wa wilaya maana anazo kesi zake nyingine. Baada ya kuzidi kumuulizia huyo afisa wa WLAC Muleba akasema hakimu amekubali kutusaidia katika hii kesi. Tukamuuliza hakimu huyo alikataa ombi letu mwanzoni je ni kwa vipi ataweza kutusaidia wakati alisema hukumu haijataja mali azoshinda mama katika kesi yake ya madai na baba. Ila katika hukumu ilitaja shamba 2 na nyumba ya kuishi ambapo mama aliamuliwa kujenga nyumba nyingine na kufanya hivyo ila hiyo nyumba ya familia ya mama kaka amewapangisha watu.na mama anaishi mitaani tangia mwaka 2006. Naomba msaada nifanyeje maana nahisi afisa wa WLAC na nguvu alizonazo kaka nahisi kuna kitu. Asante sana ...atakayeona tuwasiliane private nipo tayari.
0719815018
 
Back
Top Bottom