Msaada juu ya mbegu za mahindi,

ALF

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
207
137
Habari zenu wakuu, naomba kupata muuongozo juu ya swala lifuatalo, shambani kwangu nimefunga mfumo wa umwagiliaji kwenye hekari moja na makusudio yangu ilikuwa ni kupanda tikitimaji ila niliingia hofu kutokana na hali ya hewa mwezi january hivyo nikapanda bamia, kwasasa naona zinaelekea ukingoni, wazo la kupanda tikitimaji bado ninalo, ilaniliwaza nipande mahindi kwajili ya biashara kwa watu wanaochoma ili niweze kuwauzia nilipiga hesabu kama nitakuwa na kiche 20,000 X 300 kwa bei ya soko = 6,000,0000/= ningehitaji mbegu inayozaa mahindi mawili na inakomaa baada ya siku 70.

Baada ya maelezo marefu naomba ushauri wenu kwa mwenye uzoefu na kilimo hiki cha mahindi mabichi au nayefahamu anisaidie ni mbegu gani ya mahindi ambayo ni 1, kubwa, 2. Inabeba mawilimawili, 3 inakomaa ndani ya siku 70 - 75 ., 4.Mahindi yake yanaradha na yanauzika sokoni , ili niweze kutafuta mbegu hiyo nitakapoto bamia niweze kupanda.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom