Upande wa Alibaba naona hawaruhusu kununua kitu kimoja hivi vidogo vidogo.Banggood in reputation mbovu sana, wanaweka listing ya items nyingi ambazo hawana kwenye stock. www.gearbest.com wana uhafadhali kidogo lakini pia ningekushauri uizoee Aliexpress maana wana team ambayo ni wazoefu. Kuhusu swala la kuchelewa kwa bidaa/items wakati mwingine ni uchumi tu, unapolipia usafiri wa posta za kawaida kama Hong Kong Post au China Mail kuchelewa ni lazima tofauti na ukatumia courier service kama DHL au FedEx. Jitahidi ujipange wakati wa project unaagiza vifaa vingi kwa wakati mmoja ata kama ni kwa ajili ya multiple projects vitakua bundled kwenye package moja na utume kwa courier service, kimahesabu inaweza kuwa nafuu zaidi. Pia ukumbuke nature ya e-commerce nchini China ni kuwa siyo kila anaelist items online anakua na stock ya hizo items, wengi wanafanya backorder baada ya wewr kulipia, so anaweza kuwa Beijing kiofisi lakini items anachukua Shenzhen kwa hiyo chances za delays zinazidi kuwa juu.
utaenda utarudi Aliexpress ndio baba lao, hapa naongelea wingi wa items
kuhusu kuchelewa kwa bidhaa, , muuzaji ndio anahusika na sio iyo platform ya uuzaji, muuzaji uyo uyo yupo Ebay, yupo Aliexpress, yupo Bangood, yupo Amazon, yupo Gearbest
kama hulka yake ni ku back-order na kuku tumia, atachelewesha ivyoivyo haijalishi anatumia platform ipi
ukija kwa shipping, kuna classes pale, kulingana na mfuko wako
kuna Economy, Standard na Express,
kwa mizigo ya 'kawaida' Aliexpress( au Ebay,Bangood,Gearbest ), ukichukua standard shipping ya $ 3.0 ivi, delivery inakua around 2 weeks ( China to Posta Kuu )
kama una mizigo midogo ya kuagizia mfano: resistors, ICs, microprocessors sijui diodes ( sana sana najua unaweza usizidi 1kg ), unaagizia vingi kwa mkupuo then unatumia Alibaba
Kwa DHL hua inagonga $ 50 flat kwa izo takataka ( hazizidi 1kg) , ndani ya siku 6 vinatua AirPort pale, mimi binafsi hua nafanya ivyo
pitia huu uzi hapa, kama unataka kununua mwenyewe bila 'wakala', kuna kila kitu kwenye uo uziMtaalam hivi hawa Aliexpress wana mawakala wa kusambaza vitu tunavyoagiza mtandaoni kama kikuu? Maana sisi wa mikoani kikuu wanatufikia kwa urahisi.
Vipi kuhusu kodi ya vitu vidogo vidogo kwa upande wa Aliexpress?
Sent using Jamii Forums mobile app