Wakuu nimerudi jana tu kutoka Ruvuma, kwa kweli idadi ya gariza IT zilizomalizikia njiani kwa hesabu za haraka haraka zilifika sita. Hii ilinilazimu kumuuliza dereva wangu hii inasababishwa na nini, dereva wangu kumbe naye kabla ya kupata ajira rasmi alishawahi kufanya kazi kama hizo tena kwamalipo mazuri (si chini ya laki mbili).
Anasema tatizo mmiliki wa gari la IT anajikuta anatafuta dereva wa bei chee vijiweni na kukwepa wale wazoefu, matokeo yake wanajikuta furaha yote ya kupeleka gari nyumbani inaishia porini, na kibaya zaidi hata na maisha yao yanaishia hapo hapo.
Barabarabi kuna changamoto nyingi zinataka dereva uwe na uzoefu wa kutosha kwanza ukianzia na barabara husika pamoja na ozoefu wa kutosha wa tabia ya gari lako (Zijue breki zako kwa ufasaha, tairi zako na life span yake, upepo wake uko sahihi kw asafari ndefu kama hizo nk).
Ndugu mtoa mada nafikiri utakuwa umepata pakuanzia utafiti pia, sio tu kila gari upande je na uzoefu wa dereva kwa safari kama hizo upo?