Msaada juu ya Hearing Aids!

Msaada juu ya Hearing Aids!

Rais Msomi

Member
Joined
Jul 28, 2017
Posts
53
Reaction score
67
Habari Wandugu wa Jf!!


Ndugu naomba msaada wa haraka kwa mtu yeyote ambaye ana uzoefu wa kutosha ama amewahi kutumia Hearing Aids kwani nina matatizo ya masikio.

Last week nimefika KCMC,nikaonana na Specialist wa Kitengo cha ENT,kwa kuwa ilikuwa Rufaa alifanyia check up na baadaye akanielekeza kwenda kupima.

Baada ya Vipimo mle chumbani, technologist aliyenipima aliniambia masikio yangu yana tatizo na hivyo solution ni hearing aids.

Akasema kwa Kiwango cha tatizo ililonalo unapaswa kulipia Laki3 kwa masikio yote mawili.

Nimesikia Hearing Aids zina challenges zake ...Tafadhali kwa mtu mwenye utalaamu nazo anipe ushauri kabla ya kwenda kuzichukua.

Natanguliza Shukrani!!
 
Kweli huwa zinakuwa na challenge sana, Huwa kila aina ya sauti hunasa kwa haraka, mfn mtu akiwa nyuma yako umbali km wa mt7 hivi akiwa kwenye floor basi km ataburuza miguu yake wewe utahisi kelele sana
 
Kama una picha ya hivyo vifaa ambavyo umeambiwa vinagahrimu hiyo pesa iweke hapa ili upate maoni vizuri kwani vifaa vipo vya aina mbali mbali


Kwa bahati mbaya sina picha yake.Kwani hakutaka kunionesha mpaka niwe na hela.Nina mpango wa kurudi kesho labda naweza kumuomba nivione kabla ya kuchukua maamuzi ya kuvinunua.
 
Habari Wandugu wa Jf!!


Ndugu naomba msaada wa haraka kwa mtu yeyote ambaye ana uzoefu wa kutosha ama amewahi kutumia Hearing Aids kwani nina matatizo ya masikio...
Tatizo la madaktari wetu hawaangalii tatizo lako la usikivu lipo vipi kwa mfano unaweza kuta tatizo lako lipo upande wa kuelewa nini watu wanazungumza.

Sasa unapewa kifaa ambacho kazi yake kuvuta sauti tu mwisho wa siku kinakuwa hakuna msaada wowote.

Changamoto kubwa ya hivyo vifaa ni utunzaji kwa maana visiingie maji tu
 
Masikio yangu yana kelele nyingi mno...sasa kwa maelezo yenu hapo juu nakuwa bado niko kwenye dilemma....

Juu ya kipi au uamuzi gani nichukue!!
 
Habari Wandugu wa Jf!!


Ndugu naomba msaada wa haraka kwa mtu yeyote ambaye ana uzoefu wa kutosha ama amewahi kutumia Hearing Aids kwani nina matatizo ya masikio...
Waswahili bhana! Sasa katika Kichwa chako cha Habari umeandika kwa Kiingereza na cha Kushangaza huku katika uzi wako sasa kamili sehemu nyingi kama siyo kubwa umetumia lugha ya Kiswahili sasa sijui hapa tukueleweje? Watanzania mkisoma na kuelimika kidogo huwa mnakuwa na ' taabu ' sana hakyanani.
 
Nadhani Vifaa vyenyewe vinafahamika hivyo!!

Nadhani ujumbe wake uko wazi ungeweza tu kusaidia hata bila kuona lugha iliyotumika ni kikwazo kwako.

Naomba msaada ndugu yangu Gentamycine!!
 
Mkuu nakushauri mwambie akuandikie hivyo vifaa. halafu usinunue, nenda kafanye vipimo hospitali nyingine mf. CCBRT / Bugando / Muhimbili. Kisha linganisha majibu utakayopewa. Hakilisha mpaka umejiridhisha kuwa hiyo ndio njia ya pekee ya kutatua tatizo lako, basi ndio uvinunue.
Usiogope gharama za kupima upya mahali pengine!
Hizi hospitali zetu tunazijua wenyewe!
 
Masikio yangu yana kelele nyingi mno...sasa kwa maelezo yenu hapo juu nakuwa bado niko kwenye dilemma....

Juu ya kipi au uamuzi gani nichukue!!
Kama yana kelele hizo hearings aids hazitakusaidia endelea kutafuta suluhu nyingine usipoteze pesa kununua hizo aids mpk pale kelele zitakapokata
 
Masikio yangu yana kelele nyingi mno...sasa kwa maelezo yenu hapo juu nakuwa bado niko kwenye dilemma....

Juu ya kipi au uamuzi gani nichukue!!
Yes inabidi dr akwambie in detail maana unaweza chukua healing aid ambayo haikufai ila ikamfaa mtu mwingine
 
upload_2018-2-22_10-36-54.jpeg
upload_2018-2-22_10-36-54.jpeg
 
Habari Wandugu wa Jf!!


Ndugu naomba msaada wa haraka kwa mtu yeyote ambaye ana uzoefu wa kutosha ama amewahi kutumia Hearing Aids kwani nina matatizo ya masikio.

Last week nimefika KCMC,nikaonana na Specialist wa Kitengo cha ENT,kwa kuwa ilikuwa Rufaa alifanyia check up na baadaye akanielekeza kwenda kupima.

Baada ya Vipimo mle chumbani, technologist aliyenipima aliniambia masikio yangu yana tatizo na hivyo solution ni hearing aids.

Akasema kwa Kiwango cha tatizo ililonalo unapaswa kulipia Laki3 kwa masikio yote mawili.

Nimesikia Hearing Aids zina challenges zake ...Tafadhali kwa mtu mwenye utalaamu nazo anipe ushauri kabla ya kwenda kuzichukua.


Natanguliza Shukrani!!


Mkuu pole sana kwa tatizo hilo lililokupata.Kifaa kwa kiswahili kinaitwa SHIME SIKIO (HEARING AID)

Kifaa hicho huwa kinatumika kukuza mawimbi ya sauti katika sikio la msikilizaji.Ni kweli kifaa ghari.Pia vipo vya aina nyingi kama vile pocket hearing aid na vingine unavaa kama miwani ya jua au kusomea.

Vifaa hivyo vinawafaa watu wenye matatizo ya usikivu mdogo. Angalia majibu ya Daktari aliyekupima kama yanawiana na kiwango cha usikivu kati ya viwango hivi ndo utaweza kubainisha kama unaweza kutumia hicho cha hearing aid au la
  • MILD HEARING LOSS
  • MODERATE HEARING LOSS
  • SEVERE HEARING LOSS
  • PROFOUND HEARING LOSS
Mara nyingi watu wenye matatizo hapo MILD HEARING LOSS huwa ndo wanatumia hivyo vifaa na vikawafit vizuri lakini kutegemeana na mazingira waliyopo wao.Kwa mfano katika nchi za wenzetu kuna mazingira ya utulivu namaanisha MAKELELE ndo maana vinawafaa sana sasa kwa sisi Tanzanani kila sehemu makelele matokeo yake ukivaa hicho kifaa utajiumiza wewe mwenyewe na wala hakitakusaidia kitu chochote labda tuseme shuleni lakini si katika maeneo ya wazi.
Kwa mtu mwenye kiwango cha usikivu Mkubwa kidogo (MODERATE HEARING LOSS) akitumia kifaa hicho kitamsaidia kidogo sana.Kwa wale wenye SEVERE NA PROFOUND HEARING LOSS Hawashauriwi kutumia hivyo vifaa maana huwa havina msaada wowote kwao hasa Profound hearing loss yaani ni totaly deaf wao utumia LUGHA YA ALAMA katika mawasiliano yao yote.


Binafsi sikushauri kabisa kutumia hivyo vifaa kwa kukurupuka maana ukivitumia utazidi kupoteza kiwango chako cha usikivu ambacho cha sasa ni bora zaidi ni afadhari ukabaki hivyo hivyo huku kidogo unasikia.Kumbuka vifaa vilitengenezwa kwa mazingira ya ulaya kwa wenzetu huko ambapo kuna sheria za air pollution nk Sasa unataka kuvitumia hapa kwetu ni kujitakia majanga zaidi mwenyewe.
Unaweza kufanya kautafiti kadogo kupitia kwa viziwi ambao walitumia vifaa hivyo na sasa wanajisikiaje?Mwisho kama una wasiwasi unaweza kutembelea shule ya viziwi Buguruni wana audiology clinic,Muhimbili na hapa Moshi unaweza kuwaona wadau wa viziwi wakushauri zaidi kuhusu hivyo vifaa pia ukitaka msaada kwangu ni PM
 
nauza hearing aid kifaa cha kuongeza usikivu , pia inasaidia kupunguza kelele maikion bei laki 4 dar gongolamboto 0684340704 sikio la kushoto

260966093_423917225935164_1713326625828392898_n.jpg


262951240_423917055935181_1730805183640467547_n.jpg
 
Back
Top Bottom