Msaada juu ya chafya

Msaada juu ya chafya

ICHANA

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
4,765
Reaction score
3,596
Wana JF, naombeni ushauri kama kuna mtu amewahi kuwa na tatizo kama langu au hospital gani naweza pata tiba.

Nina tatizo la kupiga chafya limenianza around miezi kadhaa sasa naona kama kero na huenda kuna tatizo sehemu.

Nakuwa napiga chafya mfululizo hata kumi kwa wakati mmoja wakati mwingine wa chafya pua zinakuwa zinawasha ndani na mafua ambayo ndani ya dakika kumi na tano narudi hali yangu ya kawaida.

Na huwa inatokea asubuhi mara napoaamka, au ile natoka kuoga, na mchana.
 
Nadhani ni allergy kuna rafiki pia yuko hivo kila asubuhi mchana mzima.Sijui matibabu yake exactly ila rafiki yangu huwa anatumia cetrizine kidonge kimoja kabla ya kulala.
 
asante mkuu cetrizne ndo nlipwa nA dr ila sion nikipona wala unafuu ...inaweza kupita siku nzima bila chafya na siku nyingine inakuwa kama sifa .allergy kama ni haruf kali au vumbi nadhani ingetokea zaid na hyo mazingira .au nakosea labda niulize kama allergy inaweezkana inatokea muda wowote hta kama hkuna harufu au vumbi??
Nadhani ni allergy kuna rafiki pia yuko hivo kila asubuhi mchana mzima.Sijui matibabu yake exactly ila rafiki yangu huwa anatumia cetrizine kidonge kimoja kabla ya kulala.
 
Mkuu hata mimi hilo tatizo la kupiga chafya ndo limeninyima raha huku duniani, naweza kupiga chafya hata kama ni usiku wa manane na ni mfululizo hadi mapafu yanauma. Tena zikiamka ni popote tu haijalishi niko katika mazingira gani. dr alinishauri nitumie piriton pale zinapoamka ila naona hazinisaidii tena.
 
Mimi nimeishi na hiyo hali kwa takribani miaka 20 bila ya kujua kuwa nina tatizo la alergy,ila baada ya kupata ushauri wa daktari ndio nikajigundua kuwa ni alergy, kuna dawa nzuri sana inaitwa Celestamine,

unameza kidonge kimoja asubuhi na jioni,nakumbuka nilianza na vidonge 30,baada ya kumaliza ndio akaniambia kuwa inapotokea tena ndio unatumia dozi ya siku mbili au tau then unasonga na maisha,

kiukweli zile chafya za asubuhi ni almost zimekata kabisa,shida yangu huwa nikakaa kwenye Ac muda mrefu au kuna baadhi ya perfume nikitumia huwa zinaniletea shida au hata nikikaa sehemu yenye mavumbi huwa napata hiyo hali ya kupiga chafya sana.Ushauri,tafuta specialist wa ENT(Ear,Throat na Nose) atakupa msaada mzuri sana.
 
Nenda hospital yoyote ya gvt ndo muhimu zaidi suala lako ndogo sana!
 
hili tatizo lilinisumbua ila baadae nikagundua inasababishwa na harufu ya mti fulani manake nilikua nikiondoka eneo ninaloishi zinapotea nikirudi napiga chafya mpaka kichwa kinauma.
 
Kwa mujibu wa maelezo yako utakuwa na mzio (allergy) na kuna kitu kinasababisha hiyo hali inaweza kuwa sabuni au hata mazingira unayoishi kama vumbi jepesi kwa sababu chafya ni mechanism ya wili kuondoa irritation kwenye pua baaada ya taarifa kutumwa kwenye ubongo (sneezing centre) na kupiga chafya kuondoa hiyo hali. Jaribu kubadili aina ya sabuni uone matokeo yatakuwaje.
 
asante mkuu ntajaribu hizo dawa naamini nami
ntapona
Mimi nimeishi na hiyo hali kwa takribani miaka 20 bila ya kujua kuwa nina tatizo la alergy,ila baada ya kupata ushauri wa daktari ndio nikajigundua kuwa ni alergy, kuna dawa nzuri sana inaitwa Celestamine,unameza kidonge kimoja asubuhi na jioni,nakumbuka nilianza na vidonge 30,baada ya kumaliza ndio akaniambia kuwa inapotokea tena ndio unatumia dozi ya siku mbili au tau then unasonga na maisha,kiukweli zile chafya za asubuhi ni almost zimekata kabisa,shida yangu huwa nikakaa kwenye Ac muda mrefu au kuna baadhi ya perfume nikitumia huwa zinaniletea shida au hata nikikaa sehemu yenye mavumbi huwa napata hiyo hali ya kupiga chafya sana.Ushauri,tafuta specialist wa ENT(Ear,Throat na Nose) atakupa msaada mzuri sana.
 
HII KITU INANISUMBUA SANA..
 
asante mkuu ntajaribu hizo dawa naamini nami
ntapona
Ukitumia dawa tu bila kwenda kumuona specialist sio vizuri.
Ni vema ukamuone specialist akufanyie vipimo vya kueleweka sio kubahatisha.
Pia usiende kwenye zahanati za mtaani nenda kwenye hospitali kubwa za kueleweka.
 
Wakati unafanya mapenzi ghafla ukabanwa na chafya... Game itaendelea kweli?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom