ISP ni Internet Service Provider. Hapo kwene Ipad kuna mini-SIM card ndio itayofanikisha kukuunganisha na www. Kama huna bado hiyo mini-SIM waone Voda / tIGO / Airtel etc etc. Kuhusu kuongeza salio itabidi uitoe hiyo mini-SIM na kuiweka kwene simu ya kawaida kisha unaingiza vocha kama kawa, halafu uta-invoke package unayoitaka ya internet ( ISP wenyewe watakupa maelekezo).
Kuhusu iTunes ID, inabidi kadi yako iwe active kutumika online. Waone watoaji wa card yako (benki) wakupe maelekezo.