Msaada: Jinsi ya kusafirisha samaki bila kuharibika

Feb 22, 2015
21
6
Nataka nianzishe biashara ya samaki kutoka kanda ya ziwa kuja arusha na kilimanjaro naomba msaada wa njia za kusafirisha samaki bila kuaribika kwan mtajio wangu ni mdogo bado cjaweza kumiliki gari kwaajili ya kusafirishia
 
Wa jina embu rejea topic ya biology ya natural preservatives kama sijakosea. Kama ni samaki unaweza ukatumia chumvi nyingi halafu ukatafuta matenga ukawapanga vizuri. au pia waweza kuwakausha kule kule mwanza ili kupunguza uwezekano wa kuharibika.
 
Inategemea unasafirisha wakiwa katika hali gani. Unaweza kukausha au kusafirisha wabichi na pia njia zote zina changamoto zake. Ukikausha lazima ujue walaji au soko lako linahitaji nini, mfano unaweza kausha sana au kwa kiasi kidogo tu, ukikausha sana ni hawatawahi kuoza na unaweza kusafirisha mbali zaidi. Ukisafirisha wabichi utahitaji freezer(Jokofu) na pia unahitaji kuwa na barafu za ziada kwa kulinda ubaridi, unaweza pakia ktk jokofu Mwanza na pia una tafuta mtu akuandalie vibarafu na ukifika labda Singida unaviweka ndani unaboost coldness mpaka A-town. unaweza pia fikiria kwa njia tofauti ila nadhani haya ni yamsingi ni wewe tu kuboresha.
 
ahsante kwa ushari wako ninaufanyia kazi kaka
 
Wa jina embu rejea topic ya biology ya natural preservatives kama sijakosea. Kama ni samaki unaweza ukatumia chumvi nyingi halafu ukatafuta matenga ukawapanga vizuri. au pia waweza kuwakausha kule kule mwanza ili kupunguza uwezekano wa kuharibika.
ahsante broo
 
Kikubwa hapo ni uhitaji wa soko na gharama za uhifadhi. Sina uhakika kama TFDA wana miongozo juu ya viwango na ubora wa njia hizi? unaweza ukafuatilia pia kuepusha karaha pale utakapo kaguliwa na wahusika.
 
Njia nyingine pia ni kuwakaanga.

Kama una kamtaji kidogo jikoki ununue vifaa vya kukaangia, ukiweza kuwakaaanga unaweza wasafirisha umbali mrefu kwa risk ndogo sana ya kuharibika.
Na muitikio wa wateja sokoni kwa samaki wa kukaanga uko juu sana
 
Biashara ya uhakika na endelevu safirisha wabichi ,kama utachukulia musoma pale kuna freezer za kukodi kwa ajili ya kugandisha samaki then unawasafisha kwa malori ya mizigo ambapo kwa sasa bei ya kuusafirishia kg mmoja musoma to Arusha ni tsh Mia mbili, kama utachukulia mwanza pale kuna coldroom za kugandisha samaki kabla hujawasafirisha
 
Una fununu za jinsi ya kusafirisha samaki kutumia dawa ya kuhifadhi maiti. Unatamani kweli watu wajitokeze kuelezea.

Ndiyo wale wale wanao omba dawa za kaputi kwamba mbwa anaumwa wanataka kumtibu.
 
Kaka mimi nipo mwanza nafanya biashara ya samaki wabichi na kila siku tunasafirisha samaki kwenda sehem mbalimbali ikiwemo Arusha na wanafika wakiwa vizuri pia nina mpango wa kufungua bucha moshi ntakua nauza jumla na rejareja unaweza kuwa mteja wangu,karibu sana
 
Mkuu hizo leseni sio gharama sana, maana inapofika suala la kukata vibali serikali ta Yanzania hilo suala linakua pasua kichwa
kuhusu gharama za leseni sijui wanalipia kiasi gani lakini kibali ambacho unakitumia kusafirisha mzigo husika gharama yake ni ndogo sana,lakini unatakiwa kuwa na leseni ya kufanya biashara husika then ukitaka kusafirishia mzigo unaomba kibali maliasili
 
Sio lazima uwe na kibali kama una mtu yupo mwanza then anakutumia mzigo we unasubiri kupokea mzigo wako tu
 
ukikamatwa na kasi hii ya magufuli ndio utaelewa hata wengi wanafanya hivyo lakini sio utaratibu so ni uamuzi wako tu.
 
Back
Top Bottom