Ni suala jepesi.
1. Menya viazi/ndizi zako,
2. kata slesi nyembamba. Ni vizuri kutumia kifaa maalumu cha kukatia slesi nyembamba,
3. osha kwa maji safi,
4. weka chumvi kiasi kidogo kisha loweka kwenye maji (yawe usawa na viazi/ndizi zako) kwa muda wa dakika 20,
5. mwaga maji uliyolowekea,
6. weka mafuta kwenye kikaango kisha bandika jikoni, yakipata joto la kutosha weka slesi zako na anza kukaanga ukizigeuza mara kwa mara. Usisahau kunionjesha jaribio lako la kwanza.