Msaada: Jinsi ya kupata Visa - Dubai

Uzuri wa dubai work permit unataftiwa na aliyekuajiri,

Ninaweza nikakuunganisha na mtu akakutaftia maana kipindi niko dubai nimekaa hata abu dhabi, sharja ,fujaira na maeneo kibao,

Hivyo ni pm au nipate kwa simu nadhani namba yangu unayo,

Yaan we ukipata visa ukapata kazi anayekuajiri ndo anakutaftia permit ya kuishi na kazi, kwa dubai, hata nchi nyingine ni hivo, ila kwa baadhi ya nchi unakuta waajiri hawana uwezo mnashare gharama,

Ila sasa huyu atakayekupa visa utamuongezea yake ya soda badala ya 200 anaweza kataka 300 USD
 
Ngoja nikutafute sasa hivi Boss
 
Hongera mkuu kwa kuchukua maamuzi kama hayo.

- La kwanza hakikasha unachukua visa ya miezi mitatu, (wiki mbili ni ndago sana kwa ishu ya kutafuta kazi)
- tafuta mtu dubai au zanzbar akotolee visa inapatikana kwa urahisi sana, na nafikiria pia kwa kupitia ndege zao Emarates au Fly Dubai mazingira ya visa yanarahisika zaidi ungejaribu pia kwenda kwenye ofisi zao.
- Visa inapatikanwa baada ya siku tatu za kazi ndio taratibu hasa ukipata mtu wa kule. (hao wasiku 14 niwasumbufu tu)
- guest house average bei ni 45 - 50usd a day hiyo ndio chepest utakayopata. (kwaiyo ukifikia ujiandae kabisa masuala ya kutafuta sehemu ya bed space ili usikae masiku hoteli.
- Gold Plaza, naif road at gold souk, Deira. Queen hotel sabha road, Deira. Naif view hotel, Deira. Dowan town nayo pia Deira. (ni baadhi ya Guest house unazoweza kufikia ikiwa utakosa mwenyeji, bila ya ivo unaweza kuja kujikuta umeangukia hotel ya bei kubwa, Na pia imagration wakikuona mpya mpya unashangaa shangaa wanaweza kukubana kukuuliza wapi unafikia kwiyo uwe namajibu yakuwapa)
- Na kuhusu unapopata kazi. Kwa ufahamu wangu nahisi kitaratibu itakubidi urudi huku baada ya kupata kazi halafu uwende tena. Mara nyingi wao hukutumia ticket japokua wengine hukukata kidogodogo kwenye mshahara. (na masuala ya work permit wnashuhulikia wenuewe waajiri)
- Hakikisha una pesa ya kutosha ya hakiba.
Ila mwanangu ukifanikiwa kupata kazi dubai ushatulia kabisa. Straggling miaka miwili ya mwanzo zitakuepo jiandae nazo kwaiyo uvumilivu unahitajika unless ule Bingo kazi ya maana. Lakini mara nyingi watu wengi kazi ya mwanzo inakua yakuanzia maisha tu pale, lakini kila utakavokaa utapata uzoefu wa jiji na opportunity nyingi utaziona. Ugumu wa Dubai ni ile starting point.
- Na dubai uwe makini sana kufata sheria kila kitu faini ikikushinda unatiwa ndani, usije kuja kujitia kwenye basi la abiria au train bila ya kadi tena yenye kiwango cha pesa kinachotakiwa utaumbuka mkuu.
 
Ahsante sana Mkuu,nashukuru kwa darsa la kutosha Boss,nimepata mwanga kwa kiasi kikubwa Boss,shukrani sana!!.
 
Siyo mpaka arudi huko, anaweza aka exit kwenda nchi ya karibu, zamani walikuwa wana exit kwenda Quesh iran, na nchiI jirani ili visa itoke, maana haiwez kutoka kama uko ndani ya UAE
Anaweza enda India au oman, au nchi ya karibu na hapo,

Ila umempa nondo nzuri sana
 

walikua wanatumia sana kwenda Oman. Ila nilisikia sikuhizi pia inaleta usumbufu sasa sijafatilia bado usumbufu wa aina gani.
 
Mnaendelea kunifungua sana akili Mkuu, haya mambo nisingeyajua kama ningeamua kukaa kimya na kufanya siri,ahsanteni sana Wakuu,ipo siku nina imani nitakuwa na share experience kwa wengine pia.
 
DUBAI uwe makini tu mkuu, mwenzio nimepindwa miaka mitatu nimerudi mifuko mitupu. Pesa yote nimeimalizia kwa madem na misosi.

Wasomali, Waethopia, Wanigeria, Wakenya, WaLebanoon, Wahindi, waphilipino, waTunisia kiufupi vurugu tupu. Kama sie watoto wa Dar tumezimaliza hukohuko tumebakisha kutoa stori tamutamu tu vijiweni. ili uinusuru pesa yako ukitoka job ujifungie ndani tu.
Na kuhusu misosi yani we acha tu.
 
Hahaha nimejikuta nacheka Mkuu Pole sana aisee!!.
 
Kwl Mkuu,ndiyo maana nimeandika kama kuna mtu aliyeko Dubai angenipa taarifa kamili ingenisaidia sana!!.
Why Dubai? Usinijibu mimi nakupa formula ambayo mie hutumia. Jiulize hilo swali over and over ukiona huna hata chembe ya doubts. Proceed. All the best bro.
 
good
 
Jamii inataka watu kama nyie. Safi mkuu!
 
Mkuu Dukeson habari, je ungependa kushare nasi mrejesho wa hii post kwa faida ya wengine?
 
Hii story naipata wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…