Msaada: Jinsi ya kulima matikiti ili nisipate tena hasara

Msaada: Jinsi ya kulima matikiti ili nisipate tena hasara

ntera

Senior Member
Joined
Jul 23, 2009
Posts
139
Reaction score
44
Habari wadau!Poleni kwa mihangaiko ya siku nzima.
Naomba niende mojakwamoja kwenye mada. Nina shamba ekari 3 ambazo niliamua mwaka huu nilime matikitimaji.
Niliweka mifumo karibia yote (kwa ufahamu wangu). Kwenye shamba langu kuna mto ambao ni wa masika tu, kipindi ambacho sio masika mahali pangu tu ndio kunatuama maji, kwa hiyo mimi napata maji mwaka mzima,

Sasa basi nimenunua pump na kujengea tanki la lita 5000 ambalo ndio najaza maji kwa ajili ya umwagiliaji, (sijatandaza mipira mpaka kwenye mashimo).

Kwenye Hilo shamba nimeweka mfanyakazi kulihudumia shamba lakini cha ajabu juzi kanitumia msg kuwa matikitimaji hayajazaa na hakuna jinsi sababu anayotoa ni jua kuwa kali.

Naomba mnishauri jinsi ya kulima ili nisipate hasara tena kwa wale ambao walishalima hili zao wanajua ni hasara kiasi gani mtu anapata akilima ekari 3 ya matikiti ambayo hayakuzaa.

Nini nilikosea nirekebishe wapi ili yasinikute tena.

Natanguliza shukran.
 
Matikiti hasa yanataka jua, ila huyo mtt wako hajayamwagilia maji ya kutosha, na pia upige dawa kuzuia wadudu wasigonge maua yanapoalikA, ila muhimu maji hasa hiki ndio kilindi kizuri cha kupanda, pole kwa hasara, pia angalia mbolea unapopanda , kama kali sana inaweza kusababisha yakakosa afya, na usisahau kutmia booster regularly
 
Umetumia msg na kijana wa shamba, hujaenda kuangalia ujue nini kimetokea??
 
Habari wadau!Poleni kwa mihangaiko ya siku nzima.
Naomba niende mojakwamoja kwenye mada. Nina shamba ekari3 ambazo niliamua mwaka huu nilime matikitimaji.
Niliweka mifumo karibia yote(kwa ufahamu wangu). Kwenye shamba langu kuna mto ambao ni wa masika tu,kipindi ambacho sio masika mahali pangu tu ndio kunatuama maji,kwa hiyo mimi napata maji mwaka mzima,

Sasa basi nimenunua pump na kujengea tanki la lita 5000 ambalo ndio najaza maji kwa ajili ya umwagiliaji,(sijatandaza mipira mpaka kwenye mashimo).

Kwenye Hilo shamba nimeweka mfanyakazi kulihudumia shamba lakini cha ajabu juzi kanitumia msg kuwa matikitimaji hayajazaa na hakuna jinsi sababu anayotoa ni jua kuwa kali.

Naomba mnishauri jinsi yakulima ili nisipate hasara tena kwa wale ambao walishalima hili zao wanajua ni hasara kiasi gani mtu anapata akilima ekari 3 ya matikiti ambayo hayakuzaa.

Nini nilikosea nirekebishe wapi ili yasinikute tena.
Natanguliza shukran.

Wataalamu wa kilimo wanatatua shida yako faster. Humu miluzi mingi
 
Nenda kwenye makampuni yanayohusika na ushauri juu ya klmo biashara. Watakupa ushauri mzuri pa1 na kukutbelea kwenye shamba lako.
 
Mkuu ntera ningependa shamba lako lipo mkoa gani? Mimi ni mkulima wa bustani kwa muda mrefu sasa na nina uzoefu wa kutosha! Usikate tamaa kilimo ndivyo kilivyo. Ninayo mengi ya kukushauri ila kubwa zaidi ni kwamba nakuomba sana jitahidi utenge muda wa kutosha ili uweze kusimamia mambo yako hasa kwenye hii miradi ya kudump pesa nyingi kwa issue senstive kama kilimo.
Unapo anza mradi wa kilimo jiridhishe kwanza na weledi wa yule mtu unaemkabidhi usimamizi. Tafuta mtu mzoefu, kubali kugharamika. Tafuta mzoefu na sio hawa maafsa ugani wa siku hizi make wengi wao utaalam wao haupo kivitendo!
Kama upo tayari, ntakuunganisha na jamaa yangu mmoja ambaye ni mzoefu, mkweli na muwazi ili ahudumie bustani yako.
Kama hili litashindikana, basi mimi mwenyewe ntajitolea kutoa darasa kuhusu zao la tikiti kadri ya uzoefu wangu au waweza kupekua hapa jukwaani kwani nishaelezea kwenye nyuzi nyingi tu.
Usikate tamaa mkuu!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom