Asanteh sn kwa ushauriWakishatotolewa watenge Na mama yao, unaweza kuwaweka katika chumba kilicho Na joto la kutosha Na kuwapatia chakula Na maji humo. Au asubuhi unawafungia sehemu wanakuwa Na chakula Na maji.
Asante kwa elimu je vp naweza nikafanya kuku watage kwa pamoja ili kupata vifaranga wengi?Daa pole sana na umenikumbusha mbali sana pindi nilipokua sina uwezo wakukuza vifaranga kama wewe.
Lakini kukuza vifaranga ni zoezi rahisi na linalowezekana kama utakubali kuvifuatilia kwa karibu.
Kitu cha kwanza kabisa unahitaji kuvitenga vifaranga viweke kwenye chumba na kuhakikisha vinapata joto la wastani.
Njia nzuri na isio na gharama kubwa yakutengeza joto ni kwakutumia jiko la mkaa liwashe nje likisha waka vizuri liingize kwenye chumba chao.
Ni rahisi kutambua kama joto linawatosheleza ama la.
Joto linapokua kali utawaona vifaranga wakiachama midomo kama vile afanyavyo mbwa pia hutanua mbawa zao na kuachiana nafasi ukiona hivyo fungua madirisha kwa muda mpaka wawe kwenye hali ya kawaida kisha funga tena madirisha ili kuhifadhi joto kuokoa matumizi ya mkaa mara kwa mara.
Joto linapopungua vifaranga hukusanyana hapo tambua kwamba wanasikia baridi hivyo ingiza jiko ndani.
Njia hii yakutumia jiko ni rahisi kwani kama utawasha jiko usiku saa mbili hutaweka tena mpaka asubuhi cha msingi chumba kisiwe na upotevu wa joto.
Jambo la pili ni madawa.
Hakikisha unawapatia vifaranga wako chanjo ya new castle(Mdondo/Kideri),Fowl pox(Ndui) na chanjo ya Gumboro(Mbande).
Jambo la tatu.
Madawa hasa ant biotic pindi unapoona viranga vinaonesha dalili za kuumwa na tatizo kubwa kwa vifaranga ni ugonjwa wa chorera(Magonjwa ya matumbo).
Magonjwa mengi ya matumbo hutibiwa kwa ant biotic hasa OTC 20% pia ni vema ukafika kwa mtaalumu kama uko jirani nao.
Jambo la nne ni matumizi ya dawa zenye mult vitamin mfano OTC plus.Mult vitamini hutumika wakati wote kwani husaidia kuwapa vifaranga vitamini pia huviongezea nguvu.
Jambo la tano ambalo pia ni muhimu ni kuvipa vifaranga vyakula venye mchanganyiko maalumu walau kwa miezi miwili.Vyakula hivi vinauzwa madukani lakini pia kama unaweza na kuelewa mchanganyiko huo unaweza fanya mwenyewe.
Napenda kufahamu ya mayai ninayoyatenga pembeni kusubir wengne waanze kutaga yanaweza kukaa kwa pindi bila kuharibika?Vifaranga wa kienyeji ni wagumu kidogo kukua kwa haraka na hii ni asili na kimsingi asili haina tiba vinginevyo tafuta chotara.
Lakini vifaranga hawa kama watalishwa chakula chenye mchanganyiko maalumu(starter) kasi yake ya ukuwaji itaongezeka.
Kuhusu huyo aliyeuliza ni kipi anaweza fanya ili kuku watage kwa pamoja ni rahisi;
Chamsingi hapa ni lengo na naaamini katika hili lengo lake ni kuatamishia kwa pamoja hivyo fanya hivi:
Pata mayai viza ili kuku aliyetangulia kutaga anapotaka kuanza kuatamia toa yale yakwake hifadhi vizuri na umuwekee mayai viza ili kumdanganya aendelee kuatamia mayai viza asisuse.Njia hii inasaidia kuvuta subira kuku mwingine aidha aliyechelewa kutaga amalizie na akishamaliza wakati huyu aliyechelewa anaanza tu kuatamia basi muondolee yule uliyemuwekea mayai viza na kumuwekea yakwake hivyo kuku hao watakua wameanza kuatamia pamoja na utapata vifaranga pamoja.
Yaan hapo ndipo nashindwa kuelewaKimsingi mayai yenye mbegu(jogoo) hua yanaharibika kwa hata joto hili la kawaida pasipo hata kuatamiwa.
Mimi hua nakula mayai mabichi na nimegundua yai zuri na lisilo na shombo ie halijaharibika ni yai lililotagwa siku hiohio na kadiri yai lipoendelea kukaa hata utakapolila bichi huenda litakuwa na shombo ambayo hutoweza kulila.
Nikirudi kwenye hoja mi naamini yai lakuatamishiwa kwenye kuku linaweza kukaa hata siku ishirini na likawa zima.
Chukua mfano wa kuku anaetaga yai la kwanza na kuanza kuatamia akifikisha yai la ishiri hapa inamaanisha yai lakwanza kutagwa litakua limekaa siku ishirini na kimsingi wapo kuku wanaotaga mayai ishirini nakutotoa mayai yote.
Lakini kama ni mayai yakutotolewa na mashine inashauriwa yawe yametagwa ndani ya siku saba.
Mi nafikiri kuweka yai linalohitaji kutotoleshwa kwenye fridge sio sahihi kwa msingi kwamba kwenye kuna hali ya ubaridi ambayo hua na unyevunyevu na hapo ndipo tatizo lipoanzia,nafirikiri tusitafute shortcut chamsingi ni kuweka mikakati yakupata mayai ndani ya siku saba,lakini pia kuna namna yakuyahifadhi mayai kwenye trei eidha mchongoko uwe juu ama ule ule kama uviringe uwe chini hivyo fuatilia vizuri,lakini pia uwe na generator kwaajili yakudhibiti ukatikaji wa umeme,lakini pia hizi mashine zetu nazo lazima tuhakikishe ubora wake kama uko vizuriKweli ni mtihani, niliwahi kushauriwa niweke mayai yanayotagwa kwenye fridge hayataharibika, nilifanya hivyo ila matokeo hayakuwa mazuri kabisa, trei moja walitoka vifaranga watatu, na kwenye trei tatu walitoka thelathini, ila yale ambayo niliyaingiza ndani ya siku saba toka kutagwa bila kuyawela kwwnye jokofu yalitoa asilimia 80. Hivyo kwa uzoefu wangu mdogo mayai yaliyoTagwa ndani ya siku saba ndio yanafaa kuwekwa kwenye incubator. Wataalam watatupa shule zaidi.
Mimi naomba namna unaweza ukafanya ili kutunza mayaiMi nafikiri kuweka yai linalohitaji kutotoleshwa kwenye fridge sio sahihi kwa msingi kwamba kwenye kuna hali ya ubaridi ambayo hua na unyevunyevu na hapo ndipo tatizo lipoanzia,nafirikiri tusitafute shortcut chamsingi ni kuweka mikakati yakupata mayai ndani ya siku saba,lakini pia kuna namna yakuyahifadhi mayai kwenye trei eidha mchongoko uwe juu ama ule ule kama uviringe uwe chini hivyo fuatilia vizuri,lakini pia uwe na generator kwaajili yakudhibiti ukatikaji wa umeme,lakini pia hizi mashine zetu nazo lazima tuhakikishe ubora wake kama uko vizuri
Mkuu mimi naona kama lengo ni kuzalisha vifaranga ili wakue ni bora kununua kwa wanaozalisha na incubator zao huku ukiendelea ku-pata uzoefu wa jinsi ya kukuza ili uendelee kukuza biashara huku ukijifunza. Incubator ni njia nzuri zaidi ya kuzalisha vifaranga kwa wingi lakini chanzo cha mayai yenye uwezo wa kutotolewa ni changamoto sababu unahitaji kuwa na idadi ya kubwa ya kuku waliotaga mayai kwa kupandwa na jogoo ambayo ndiyo yenye uwezo wa kutotolewa. Kukusanya mayai kwaajili ya kutotolesha ni mtihani sana na pengine atokee kwenye huu uzi atuelimishe zaidi au kama kuna sehemu maalum yenye joto la wastani ambalo haliharibu mayai. Nimevutiwa na uzi maana nami ni mdau wa hii kitu.Mimi naomba namna unaweza ukafanya ili kutunza mayai
Yasiharibike ili kutumia ktk icubator
Ila mbona yai la kuku kutaga linakaa zaid ya siku saba? Na wala harialibike kwanin haya ya incubator yanaharibika sababu nin?Mkuu mimi naona kama lengo ni kuzalisha vifaranga ili wakue ni bora kununua kwa wanaozalisha na incubator zao huku ukiendelea ku-pata uzoefu wa jinsi ya kukuza ili uendelee kukuza biashara huku ukijifunza. Incubator ni njia nzuri zaidi ya kuzalisha vifaranga kwa wingi lakini chanzo cha mayai yenye uwezo wa kutotolewa ni changamoto sababu unahitaji kuwa na idadi ya kubwa ya kuku waliotaga mayai kwa kupandwa na jogoo ambayo ndiyo yenye uwezo wa kutotolewa. Kukusanya mayai kwaajili ya kutotolesha ni mtihani sana na pengine atokee kwenye huu uzi atuelimishe zaidi au kama kuna sehemu maalum yenye joto la wastani ambalo haliharibu mayai. Nimevutiwa na uzi maana nami ni mdau wa hii kitu.
Ila mbona yai la kuku la kwanza kutaga linakaa zaid ya siku saba? Na wala harialibiki kwanin haya ya incubator yanaharibika sababu nin?
Yap hapo nmekuelewa snKimsingi mashine itabaki kua mashine na kuku atabaki kua kuku japo mashine imetengenezwa kuakisi afanyavyo kuku.Lakini kwa hili utagundua kwamba mashine haijaweza kua na ufanisi kama kuku 100%.
Tena kwa wadadisi wa mambo hua wanasema hizi mashine hua hazifanyi vizuri kipindi cha joto jambo ambalo mimi sijalifuatilia hivyo sinauhakika ila kwa msingi huo utagundua kwamba mashine unahitaji pia ufahamu vizuri hasa kujifunza kwa wenye uzoefu.
Kimsingi mashine inahitaji yai ambalo halijaanza mabadiliko.Bado mi naamini kama yai linaweza hifadhiwa kwenye joto lisiloweza kuliathiri litaweza kukaa muda mwingi zaidi kabla yakuwekwa kwenye mashine.
Chukua mfano wa kanga ambaye anauwezo wakutaga mayai hata zaidi ya 70 lakini stil kama utachukua mayai yale thelathini ya mwisho ukamuwekea bado atatotoa.
Kiwa ujumla unahitaji kuweka mkazo kuandaa matetea yakutosha ili waweze kukutagia ndani ya muda muafaka
samahani mkuu umenigusa sana....naomba maelekezo kidogo juu ya kutoa hiyo chanjo,vifaranga wangu wamekufa woteDaa pole sana na umenikumbusha mbali sana pindi nilipokua sina uwezo wakukuza vifaranga kama wewe.