Msaada jinsi ya kufika chuo cha madini Dodoma

Msaada jinsi ya kufika chuo cha madini Dodoma

Kaluluma

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
474
Reaction score
622
Habari za leo wakuu,niko njiani kuelekea chuo cha madini Dodoma kutoka Mwanza,mwenye kufahamu jinsi ya kufika chuoni hapo naomba anielekeze.
1.sehemu ya kushukia
2.Nitakapopata usafiri wa kuelekea chuoni hapo.
3.Nauli ni kiasi gani
4.kitu chochote cha ziada
Natanguliza shukrani🙏🙏
 
Asa
Ukifika stand ya mabus dodoma, panda tax /daladala zinazokwenda maili mbili au msalato.

Unashukia kituo chuo cha mipango ni pua na mdomo.

Mwaka 2012 daladala ilikuwa 400 kutoka mjini tax 6,000 sasa hivi sijui imefika bei gani.
Asante mkuu,ila samahani kidogo,stendi ya mabasi nanenane au stendi ipi?
 
Umepanda bus gan?
Habari za leo wakuu,niko njiani kuelekea chuo cha madini Dodoma kutoka Mwanza,mwenye kufahamu jinsi ya kufika chuoni hapo naomba anielekeze.
1.sehemu ya kushukia
2.Nitakapopata usafiri wa kuelekea chuoni hapo.
3.Nauli ni kiasi gani
4.kitu chochote cha ziada
Natanguliza shukrani
 
...........Ukishuka stendi ya Nanenane panda daladala hadi Sabasaba stendi then chukua daladala za Mipango/Maili mbili shukia Chuo cha Mipango kwasababu mgeni chukua boda itakufikisha Madini kwa buku tu.

........Au kama umeshukia mjini daladala za mipango unazipata General hospitali au Sango hizi mara nyingi hazina usumbufu kama sabasaba.
 
Satco inashusha abiria CBE mjini,
panda boda hadi 77 stendi ni buku tu ,
then panda daladala za mipango au st gema, shukia mipango ni ni jirani na madini..
Kama hauna mzigo mzito ukishuka CBE tembea hadi 77..( unawauliza watu maana sio mbali)
Satco mkuu
 
Nashukuru mkuu
 
Asa
Asante mkuu,ila samahani kidogo,stendi ya mabasi nanenane au stendi ipi?
Stendi ya daladala ya mjini ambapo njia zote zinaanzia. Si lazima uchukue bodaboda kwani ni karibu sana, bodaboda unalipa mara mbili mwendo wa dakika tatu kuliko kwenda chuo ambapo sh 400 mwendo wa robo saa.
 
Hivi Darlux na wao wana ofisi yao Dodoma kama Shabiby au linaishia nanenane kushusha/kupakia abiria na kusepa. Pale nanenane pana gesti?
 
Hawana ofisi,
Hapana ..urudi mjin kidogo utapata malazi
Hivi Darlux na wao wana ofisi yao Dodoma kama Shabiby au linaishia nanenane kushusha/kupakia abiria na kusepa. Pale nanenane pana gesti?
 
Back
Top Bottom