Msaada! Je pressure ya macho inatibika?

Msaada! Je pressure ya macho inatibika?

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
Wasalamu jf ni platforms kubwa sana imebeba watu toka nyanja zote naomba kujua je pressure ya macho inatibika.
Nina mzee wangu ana tatizo Hilo ana umri wa miaka 83 shida ilianza miaka 20 iliyopita kwa kuanza kuvaa miwani miaka sita imepita sasa tangu aache kuona kabisa anaona mwanga mweupe hata sisi wanae anatumbua kwa sauti lakini ana nguvu tu upofu ndo unamnyong'onyesha kwa sababu ana shinda tu ndani mda wote ni chumbani sebuleni hatoki nje sababu ya Hali ya usalama pia wa pikipiki kusema afanye mazoezi so mwili hauna mazoezi upelekea hapati usingizi usiku ukesha macho.
Utalaamu na uzoefu unatofautiana naona mwenye kujua kama kuna msaada wowote wa kuweza kurejesha uoni wake maana kama ni dawa keshatumia sana Kuanzia hizi mbadala nk.
Hospital ya macho ccbrt miaka 6 iliyopita walituambia msihangaike macho yashafika mwisho huwa inatokea hii uoni ufika mwisho kulingana na umri.
But wapo wazee wenye umri mkubwa kumzidi Wana miaka 90 wanaona vizuri tu.
Wengine wanasema ni hali ya kurithi kwenye ukoo wetu wapo wanaovaa miwani wangali vijana lakini hawa ilikuwa wakati ule wanasoma na baada ya kumaliza masomo naona hawavai na simu wanatumia tu.
Pana kaka yangu mkubwa ana miaka 56 nae ameanza shida hio ya kupungua uwezo wa kuona kwa asilimia 60%.
Wengine wanasema tiba zipo kilichopo Hapo ni kusinyaa kwa mishipa tu ipelekayo virutubisho kwenye macho, inaweza ikazibuliwa ikafanya kazi.
So naomba kwenye ushauri au msaada wowote juu ya hili kwa faida ya watz wengine pia kwa sababu maandishi yanaishi.
 
Duuh Pole Mkuu,ngoja tuwasikikize wataalamu
 
Sijui Dr. Siame alikuwa mtaalam wa macho atakuwa wapi, hebu tafuta namba yake anaweza kukushauri.

Pole.
 
Back
Top Bottom