Msaada Jamani!!!!!!

mudushi

Senior Member
Oct 19, 2010
151
75
Jamani nahitaji msaada wa matibabu ya kifafa haraka. Kuna watu wananiambia kuwa tiba sahihi ya kifafa ni kwa kutumia mitishamba na si kutumia dawa za hospitalini. Sasa nimeshindwa kufanya maamuzi ya kuanza matibabu. Mwenye ukweli atoe msaada jamani. Nataka jumatatu trh 17 Oct 2011 nianze tiba.
Asanteni
 

Mupirocin

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,740
742
Tunaomba umri wako, je unahistoria ya kifafa kwenye familia yenu, kimeanza ukiwa na umri gani, wakati wa kuzaliwa ulikuwa na tatizo lolote nikijua haya nitakwambia nini cha kufanya. kifafa kinasababishwa na vitu vingi sana
 

Loly

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
510
208
ninavyosikia kifafa ni Jini na hospitali hakuna dawa hilo sio tatizo dogo ila usiende kwa waganga msogelee mungu kwa ukaribu sana nyenyekea kweli tatizo hilo litayeyuka hata bila ya wewe kujua mpenda anaweza yote
na yote yawezekana katika yeye ukiamini
 

Roulette

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
5,592
5,336
Kifafa kina sababu nyingi sana. Nenda hospitali watambue sababu ya kifafa chako. Ila kwa mwanzo wanaweza kukuandikia phenobarbital kupunguza seizure (kule kukauka kwenyewe). Ni hatari sana sababu ukishikwa wakati uko peke yako unaweza kuanguka vibaya ukaangukia na kukata mshipa wa damu, au ukaangukia moto, umeme etc.
 

Saikosisi

JF-Expert Member
May 4, 2007
528
30
Jamani nahitaji msaada wa matibabu ya kifafa haraka. Kuna watu wananiambia kuwa tiba sahihi ya kifafa ni kwa kutumia mitishamba na si kutumia dawa za hospitalini. Sasa nimeshindwa kufanya maamuzi ya kuanza matibabu. Mwenye ukweli atoe msaada jamani. Nataka jumatatu trh 17 Oct 2011 nianze tiba.
Asanteni
nenda hospitali, mitishamba haitakusaidia. na kifafa sio jini. kha!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom