Kuomba msamaha inategemea na aina ya kosa, uzito wake na mazingira ya kosa lenyewe bila kusahau mtu uliyemkosea ni wa aina gani kitabia. Je huko nyuma ulishawahi kufanya kosa la aina hiyo na ukaonywa lakini umerudia kosa lilelile au linalofanana na hilo ulilotenda? Hakuna kitu kinachokela kama mtu kushindwa kujitambua na kushindwa kuthamini msamaha unaotolewa kwako hasa kwenye maswala ya mahusiano. Watu wanaosamehe kirahisi mara nyingi huchukuliwa poa sana kwamba "atanisamehe tu". Lazima umpe jambajamba ndio heshima iwepo.