Msaada Jamani

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,467
14,314
Habari zenu wana Jamii...
Ninasumbuliwa na tatizo la kuumwa na kichwa kwa siku 9 sasa, na mara ya kwanza nilidhani ni malaria ndio inayonisumbua lakini haikuwa nilifanya medical test hospital 3 tofauti lakini sikuwa na tatizo lolote.

Tatizo ambalo nimeligundua sasa ni kwamba nikiongea na simu kichwa kinakuwa kinauma sana... na kutokana na kazi ninazofanya ninapiga na kupokea simu nyingi sana kwa siku(zaidi ya simu 35) na mazungumzo mara nyingi ni zaidi ya dakika 3 mpaka 5, na usiku huwa naongea na simu mpaka masaa mawili na nusu.

Jamani nahitaji msaada ninaweza kukabiliana vipi na hali hii.. au kama kuna tiba yoyote au chakula ninayoweza kutumia ili kuikabili hii hali. maana nikipigiwa simu tu naanza kuchukia hata kupokea..(SIMU ZANGU ZOTE NI ORIGINAL SIO ZA KICHINA). na vilevile natumia sana kompyuta kuanzia saa 3 asbh mpaka 10 jioni na nikirudi hhome nakua na masaa kama mawili hivi ya kutumia kompyuta.

nsaidieni USHAURI, MAWAZO NA MICHANGO YENU
 
Pole sana nahisi utakuwa na tatizo la macho nilipata matatizo kama hayo nikapewa miwani nivae for six month tatizo likaisha, kingine ni maji,usipokunywa maji mengi unaumwa kichwa sana watu wengi tunasahau kunywa maji sana
 
Pole sana nahisi utakuwa na tatizo la macho nilipata matatizo kama hayo nikapewa miwani nivae for six month tatizo likaisha, kingine ni maji,usipokunywa maji mengi unaumwa kichwa sana watu wengi tunasahau kunywa maji sana

Thanx Gaga nina tatizo la macho pia kwa mwaka wa 5 sasa na ninatumia miwani kama unavyoniona kwenye avatar yangu, na maji nakunywa lita 3 daily.
Any help please.....m
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom