labda sijajua vizuri, kila nikipata kitu kizuri na ku add kwenye curt naambiwa the item does not ship to your destination, sasa hiz bidhaa zao zinakuwa shipped wapi kama huku kwetu haziji au kuna sehemu nakosea?.
Pili kwa wale mnaofamu kuhusu kodi, kwa mf. LED tv 32" kodi ntalipia sh. ngap? nikinunua nje, na je haina usumbufu?
Tatu, nahtaji na mengineyo yatakayonipa mwanga kuhusu buying online nisaidieni, ni mara ya kwanza nataka kujaribu hii kitu, pia apart from amazon na e bay ambao pia nimekutana na kadhia kama hii, je kuna web nyingine nzuri for shopping?
lengo langu nikununua flat screen tv na electronics nyingine huko nje naona ka ni cheap.
MSAADA KWA AJUAYE.
Amazon na Ebay, huwa hawasafirishi kuja Tanzania. Ni bora uumtumie mtu mwenye address ya USA.
Kama umekaa muda zaidi ya miezi 10 nje ya nchi basi kisheria unaruhusiwa kuingiza household items moja moja kama TV, radio nk bila kulipia ushuru wa VAT
Amazon na Ebay, huwa hawasafirishi kuja Tanzania. Ni bora uumtumie mtu mwenye address ya USA.
Kama umekaa muda zaidi ya miezi 10 nje ya nchi basi kisheria unaruhusiwa kuingiza household items moja moja kama TV, radio nk bila kulipia ushuru wa VAT
Sio kweli mkuu,wauuzaji wa ebay wanasafirisha bidhaa mpaka Tanzania..mnunuzi anachagua shipping method tu..on ebay search LED TV ship international,utazipata..ukitumiwa via FEDEX utalipa kwa gharama kubwa kidogo but itakua fast na uhakika wa mzigo kutopotea
Mm nmetumiwa monitor za studio na playstation 3 mzigo wng umefika bila tatizo nmelipa elfu 50 ushuru...
Ila ununuzi wa Ebay kwa vile inategemeana na muuzaji experience yangu, wengi wa wauzaji hukwepa gharama za kusafirisha kuja Bongo kwa courier.
Njia nafuu ni kwa surface mail kupitia posta, hii sidhani kama inatumika Ebay.
Mimi nipo Tanzania
Pia jaribu kutafuta discount coupons, hii itakupunguzia gharama za ununuzi kwa asilimia kubwa, pia huwa kuna daily deals hapo unaweza kununua kitu hata kwa half price ila kama wengine walivyosema Inategemea na muuzaji so before buying angalia kama wanaship kuja huku.
Kuhusu website nyingine jaribu yahoo shopping
Kwanza ni muhimu kuelewa kuwa hizi web za shopping mfano yahoo, eBay, Amazon na Alibaba na mingine mingi hawauzi vitu isipokuwa wanawakuta nisha buyers na sellers wa hizo product
Specifically sasa kuna maduka ambayo wana partnership na Yahoo na wanatumia technology za yahoo kuuza bidhaa zao
Hivyo basi jinsi ya ununuzi na bei toka duka moja hadi jingine hutofautiana mfano kitu cha dola 500 duka la Abt huweza kuuzwa 520 duka la Antonline,
Nachoweza kukushauri ni hiki, search what you want then Utakuwa directed kwenye duka husika, angalia terms of service pia angalia page yao ya Frequently Asked Questions FAQ you will learn alot kuhusu duka na service zao, usilipie chochote
Tembelea maduka mengine kufanya comparison, ukisharidhika anza kusearch discount coupons online with relations to your choice of store and product (trust me they are always out there, just dig and dig)
Mimi hununua vitu vyangu Game supermarket,lakini hutegemeana na vitu unavyohitaji namimi huwa nasubiria sana zile siku za promo kuanzia Alhamisi hadi jumapili ambapo hao Game hutoa kijarida chao kinachoonyesha bidhaa zilizopunguzwa bei,kwa huo mpango nimewahi kununua Sony Hometheatre inayouzwa 750,00te0 kwa 400,000.Laptop ya 800,000 kwa 450,000.Display unit ya 270,000 kwa 140,000,Jiko la umeme na gesi la 650,000 kwa 400,000.Manunuzi ya online sometimes ni pasua kichwa. Mie hapa nilipo nasubiria mzigo wangu toka US karibia mwezi sasa na tracking inaonesha mzigo umeshafika umetoka customs tangu tarehe 9 May. Yani nikilinganisha pressure ninayoipata + shipping ni bora ningenunua hapahapa bongo tu.
Leo nmetoa flatscreen inch 32 ushuru nmetoa laki na 30