Msaada jamani nashindwa kuuchukia wimbo wa Perfect Combo!

Msaada jamani nashindwa kuuchukia wimbo wa Perfect Combo!

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,450
Reaction score
127,624
Nashindwa kuelewa kwani kila niamkapo, ninapotembea, ninapokuwa nimepumzika tu na hata kabla sijalala usiku lazima niusikilize huu Wimbo wa Perfect Combo wa Joh Makini akimshirikisha Mwanadada wa Niger Chidinma.

Nawaombeni msaada wenu wa haraka kwani kwa jinsi nilivyoupenda huu Wimbo najikuta nashindwa hata kufanya Kazi zangu na napenda kila mara tu niwe nausikiliza na sichoki kuusikiliza.

Nikiri kwenu kuwa Mimi hata siku moja siyo Mpenzi wa hii Miziki yenu Vijana kwani ninapenda sana Miziki yangu ya Dansi hii ya akina JB Mpiana, Werrason na Kung Fu Hero Koffi Olomide ila sijui kwanini huu Wimbo wa Perfect Combo umeniteka hivi.

Akhsante sana Msanii Joh Makini na nikutakie tu mafanikio mema katika Kazi zako zote za Muziki ndani na nje ya Tanzania na kaa ukijua kuwa huu Wimbo wako umeniteka vilivyo Mimi GENTAMYCINE na nahisi naupenda hata kuliko Mke wangu. Sijui upo wapi kwa sasa Kijana nikutafute tu nikupe Zawadi yako na upako wangu wa Kizanaki na Kiyao ili uzidi kung'aa na kutisha.

Wasanii wengine wa Bongo hebu toeni Nyimbo nzuri na kali kama hiyo ya Joh Makini ya Perfect Combo kwani ni nyimbo tamu kwa kuiangalia na kuisikiliza na haichoshi. Ama hakika Joh Makini katika Wimbo huu ulitulia hasa na Wimbo wako huo UMETUKUKA.
 
Back
Top Bottom