Habarizenu wana Jf matumaini yangu muwazima wa afya. Niende moja kwa moja kwenye topic . Hivi karibuni nime 'create' blog yangu ya extension ya .blogspot ,baada ya kupitia mchakato wa kutosha hatimaye ilifika sehemu ya ku submit url for indexing and crawling , nime google vyakutosha lakini inaonekana maelezo yako juu ya uwezo wangu. Nilikuwa naomba kama kuna mtu anaweza kunielezea jinsi ya ku create na ku submit sitemap google anisaidie.
πππππ
Mkuu ni vyema ukanunua domain kwanza, kisha ukaipoint kwenye blog yako(Kwa maelezo rahisi ni kwamba nunua domain usitumie domain ya bure yenye extension .blogspot.com tafuta ambayo ni direct, yaani kama website yako ilikuwa na domain ya bure inayoitwa: mwita.blogspot.com basi iwe mwita.com n.k). Hii itakusaidia baadae utakapopata watembeleaji na post kibao, utakuwa na uwezo wa kupata huduma za matangazo mfano kutoka adsence n.k.
TURUDI NACHO:
Kwenye blog yako unaweza kwenda kwenye
Setting->kisha scroll to ->
Crawlers and indexing ->kisha
Enable custom robots.txt kwenye switch, baada ya hapo gonga
Custom robots.txt.
Haya copy yafuatayo nenda upaste pale, utauliza baada ya zoezi kamili.
Code:
User-agent: Mediapartners-Google
Disallow:
User-agent: *
Disallow: /search
Allow: /
Sitemap: https://www.mwita.blogspot.com/sitemap.xml
Altenative fungua hii link
kisha kwenye menu kuna neno (+add property) gonga hapo kisha box litafunguka chagua sehemu ya domain weka domain mfano mwita.com au hiyo yenye blogspot, Kisha shuka chini ukiwa kwenye menu utaona neno
sitemap gonga hapo box litatokea likisema add site map weka hii link,
https://www.mwita.blogspot.com/sitemap.xml
NB: Hakikisha unabadili neno mwita kisha unaweka jina la blog yako na kama umenunua domain futa neno .blogspot, ibakie jinalasite.com n.k.
Hata sasa, Komaa Kivyako!.