msaada jaman....!

msaada jaman....!

kisenya

Member
Joined
Aug 7, 2012
Posts
6
Reaction score
4
naomben mnisaidie wana jf wenzangu...me ni msichana nmedumu na my bf takriban miaka 4 mapenz yetu yalikuwa mazuri before my bf ajapata kazi now kapata kazi kanibadlikia sana mpaka siamini kama ndo yeye 2liyekuwa tunapendana na week ya tatu sasa hapokei cm yangu mpaka ni2mie namba nyingine nkimuulza ananiambia hayuko sawa akiwa sawa ataniambia sababu imefkia mpaka hatua kahama bila kuniambia naskia kwa watu tu.Naumia sana natamani ni control hii situation but iz very diffucult sielew why ananifanyia hv msaada jamani bdo nampenda sana
 
Shosti pole lakini mpaka hapo huyo jamaa fadhila zake za punda,sasa basi asi kushughulishe,kama kaona kazi ndio inayo mtia jeuri na anawezapata anaejisikia kua nae,wewe futa machozi songa mbele hata ukimfuata nibure lakuvunda hilo...
 
Muache huru usimbughudhi.. Kama kweli ni wako, atarudi tuu..! Asiporudi, basi hakuwa wako..!
 
Poleeee kwa kuwa bado unampenda sana,ila wahenga walisema akufukuzaye hakwambii...........malizia,usichukue hatua haraka fanya uchunguzi wa kutosha kujua chanzo cha mabadiliko yake kisha ukijua ni kwa sababu upendo haupo tena au amepata mwingine jiondoe mapema japo itakuumiza na si rahisi,kuliko kumlazimisha muendelee naye,kwani wanaume sikuzote wana huruma kwa wanawake kwa hiyo ukimlazimisha anaweza kukuoa kwa sababu ya huruma na sio mapenzi jambo ambalo halifai kwani ndoa lazima iunganishwe na mapenzi au upendo na si kitu kingine.Halafu pia maumivu utakayoyapata baada ya kujua kuwa mmeo alikuoa kwa sababu ya huruma na si mapenzi ni makali zaidi kuliko maumivu utakayoyapata sasa hivi kwa kuachana naye.
 
Haya ndo matatizo ya kuwa na gf/bf badala kusubiri mpaa uolewe au uowe.

Wengi yamewakuta sababu wanakihelele cha kukata viuno kabla ya siku zao :biggrin:
 
naomben mnisaidie wana jf wenzangu...me ni msichana nmedumu na my bf takriban miaka 4 mapenz yetu yalikuwa mazuri before my bf ajapata kazi now kapata kazi kanibadlikia sana mpaka siamini kama ndo yeye 2liyekuwa tunapendana na week ya tatu sasa hapokei cm yangu mpaka ni2mie namba nyingine nkimuulza ananiambia hayuko sawa akiwa sawa ataniambia sababu imefkia mpaka hatua kahama bila kuniambia naskia kwa watu tu.Naumia sana natamani ni control hii situation but iz very diffucult sielew why ananifanyia hv msaada jamani bdo nampenda sana

Hujasema mitihani ya kidato cha nne mwaka huu umepata Div. gani. halafu sio kawaida kwa binti mdogo kama wewe kuwa na boy friend bila mpangilio unatakiwa kujitunza na kuangalia hali yako kimaisha baadaye, unasema boy friend wako alikuwa hana kazi sasa kapata kazi hii ni dalili kwamba amepata wanaofanana naye, angalia masomo achana na vibwana uchwara, anayetaka kukuoa aje nyumba ajitambulishe kwa wazazi, sio hawa wanaokuchezea na kukuacha
 
Pole sana dada yangu
'
Jambo la msingi sasa la kufanya japokua linaweza kuwa gumu kwako ni kukata mawasiliano nae,hana maana sana huyo
'
Jitahidi umsahau ondoa kumbukumbu yoyote inayokukumbusha huyo jamaa,usimng'ang'anie atakunyanyasa sana,watu wengine ni wa hovyo sana!
 
wenzio wanamkatia huko mauno we waugulia maumivu,huyo tupa kule kashakua kipolo kwako hahahahaha njiwa wako kapeperuka endelea na maisha mengine.
 
To be honest, nachukia sana Tabia yetu wanaume, ya kuwaacha tuliosota nao hasa pale maisha yanapoanza kuwa na muelekeo...

Ila tatizo la girlfriends nao wakati hali si nzuri wanakuwa hawasomeki someki wanaruka ruka lakini mishe zikianza kusoma tu ndo wanaanza kukukaba wakati ameshakuumiza kichwa sana enzi za alosto,,,

Hebu tueleze vimbwanga vyako wakati hajapata kazi vilikuwaje he he he, isije kuwa unamkaba baada ya kupata mchongo na umeshamzingua sana zamani
 
"Masikini hana tabia"
sahivi kishapata na hiyo anayoonesha sahivi ndo tabia yake halisi!!!!!!!
uamuzi ni wako sasa uvumilie au uchape lapa.......
 
::
Usilaumu sana,,hujui we ungekuwa ktk nafasi yake ungefanya nini!
Take control,,maisha hayaishi leo..jiandalie kesho yako.
=
 
naomben mnisaidie wana jf wenzangu...me ni msichana nmedumu na my bf takriban miaka 4 mapenz yetu yalikuwa mazuri before my bf ajapata kazi now kapata kazi kanibadlikia sana mpaka siamini kama ndo yeye 2liyekuwa tunapendana na week ya tatu sasa hapokei cm yangu mpaka ni2mie namba nyingine nkimuulza ananiambia hayuko sawa akiwa sawa ataniambia sababu imefkia mpaka hatua kahama bila kuniambia naskia kwa watu tu.Naumia sana natamani ni control hii situation but iz very diffucult sielew why ananifanyia hv msaada jamani bdo nampenda sana

Acha kuwa king'ang'anizi, chapa lapa songa mbele na maisha yako, wewe ni binadamu kamili usitake kukamilishwa na mtu uliyekutana naye ukubwani...
 
Kama ulimpa vya ndoa kwa miaka 4 bila ndoa ujue hapo umechokwa. Yaaani mdada miaka 4 mizima ulikuwa hujagundua hatma ya mahusiano yenu....Mimi lazima niwe wazi kwa dada zetu moja epuka kuwa na mahusiano katika umri mdogo namaanisha bado hujaipata dira yako kimaisha, pili hakikisha mahusiano unayoingia yasiwe ya starehe bali yawe ya kimaisha. Mwisho ukiona miaka miwili imepita bado giza la maisha limetanda ktk mahusiano mapya moja kwa moja jiweke pembeni uangalie ustaarabu wa maisha yako.
 
Upo sahihi sana kiongozi.......ila mapenzi yana upofu flani hv, sijui huwa inatoka wapi!!!!
 
"Masikini hana tabia"
sahivi kishapata na hiyo anayoonesha sahivi ndo tabia yake halisi!!!!!!!
uamuzi ni wako sasa uvumilie au uchape lapa.......

Mmmhhh umenitisha, km kuna ka ukweli flani hv, anyway sijui...........msiwakimbie maskini jamani, nao wana tabia njema pia wakipata!!
 
To be honest, nachukia sana Tabia yetu wanaume, ya kuwaacha tuliosota nao hasa pale maisha yanapoanza kuwa na muelekeo...

Ila tatizo la girlfriends nao wakati hali si nzuri wanakuwa hawasomeki someki wanaruka ruka lakini mishe zikianza kusoma tu ndo wanaanza kukukaba wakati ameshakuumiza kichwa sana enzi za alosto,,,

Hebu tueleze vimbwanga vyako wakati hajapata kazi vilikuwaje he he he, isije kuwa unamkaba baada ya kupata mchongo na umeshamzingua sana zamani

Wewe embu edit tena, mbona unaangalia pande mbili za shilingi kwa undani hivyo................nimekuelewa sana!!
 
Pole sana dada yangu
'
Jambo la msingi sasa la kufanya japokua linaweza kuwa gumu kwako ni kukata mawasiliano nae,hana maana sana huyo
'
Jitahidi umsahau ondoa kumbukumbu yoyote inayokukumbusha huyo jamaa,usimng'ang'anie atakunyanyasa sana,watu wengine ni wa hovyo sana!

Mwache afight kidogo bwana................huenda ni wake, haya maisha ni zigzag sana yana ups and downs sana!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom