wisdom empire
JF-Expert Member
- May 5, 2017
- 337
- 288
Habari zenu wapendwa.Naombeni msaada wa Mawazo ili namimi nimsaidie aliyepatwa na tatizo maana nimeshindwa namna ya kumsaudia.Jamaa ya yangu alipata mchumba na akaenda hadi kwa wazazi wa mwanamke kuchumbia na akatoa hadi salamu( 10000) kama ilivyo taratibu za baadhi ya makabila kabla ya mahali.wakiwa ktk mahusiano na mpenzi wake ilitokea wakatofautiana kwa vitu vidogo tu na kabla hawajayaweka sawa mambo yao jamaa akapata safari na hakurudi hadi miezi minne kupita ndo akarudi.kutokana na muda mrefu uliopita bila mawasiliano jamaa mapenz na mwanamke yakawa yamepotea kabisa na hakua na hata fikra ya kuja kuishi na yule mwanamke.aliporudi mwanamke akamtafuta jamaa kupitia ndugu zake na kudai anampenda bado jamaa na amekua akimsubiri kwa muda wote huo na wazazi wanafahamu ilo.jamaa anapata ugumu afanyaje kwani hana mapenzi tena na mwanamke.naombeni ushauri wenu huyu jamaa afanyaje....