Next time ukitajiwa bei fanya reaserch japo ingia ebay uone prices zikoje. Yaani kwa bei hio unapata 7 plus na lock haina kitu brand new. Anyways, kwanza hakikisha ni lock aina ipi.
Kuna za aina tatu;
Passcode lock- inasababishwa na kutia password ya kufungulia simu mara nyingi na kufeli, ujumbe wake utakwambia "Iphone Disabled"
Network Lock- Kama simu ni brand new, wakati unaifanyia set up, itakwambia ueke simcard, na ukieka sim card sio baada ya kujisoma itakuja na ujumbe "Sim not Valid". Kama tayari ishafanyiwa set up, utaona kama kila line unayoweka itasema no service sehemu ya kuonesha mnara.
icloud lock- Hii kiboko, na kabla hujanunua simu ambayo ina icloud lock hakikisha bei unayonunua itakuwa worth utakapoenda kuitoa. Hii lock unaweza ukachezewa mchezo na fundi alokuwa sio muaminifu na anapokuona huyajui haya mambo. Lakini kuna 2 main causes za hii lock. Kwanza ikiwa mmiliki amesahau password yake ya icloud na pili ikiwa simu reported as stolen au LOST simu itakudai hio password. Ujumbe wake ni "Activate Iphone".
Inawezekana alimpelekea fundi akamsetia email ya icloud na aka activate find my iphone, then fundi huyo akatumia hio email na password akareport as stolen, ili mrudi kwake akuekeeni sawa kwa kuwachaji tena. lakini sifikirii kama atakuwa amefanya hiv.
Anyways nihakikishie ni lock/ujumbe upi unauona katika screen yako, ili nikupe njia ufanye mwenyewe.