Msaada: Intern ya udaktari

Msaada: Intern ya udaktari

BlackGold_

Member
Joined
May 31, 2013
Posts
94
Reaction score
27
Nawasalimu wote.
Nina mtoto wa ndugu yangu yupo Dar hapo amemaliza mafunzo ya udaktari..yaani medicine ila kwa sasa alichelewa kufanya application za wizara kwa ajili ya kuanza Internship yake na hivyo kuwekwa pending hadi mwezi wa pili mwaka huu (15.02.2015).
Ok point yangu ni hii..wapi anaweza kupata kazi hapo hapo Dar japo ya kujishikiza kwa muda fulani maana mimi kumtumia hela ya matumiz kila mara kwa level yake bado hainiingii akilini vizuri.
Tafadhalini wadau naomba mnipe mwanga katika hili
Natanguliza shukrani zangu.
 
tatizo hujaeleza sababu za kushindwa kuanza internship mapema; sio rahisi kupata kazi ya udaktari bila kupita internship kwani kwenye internship ndiko daktari anakopikwa; mwambie anze mapema kwani huko wanalipwa mashahara wa 80% wa daktari.
 
Nashukuru mkuu joka.
Sababu za yeye kutoanza internship mapema ni kwamba alichelewa kuomba. Na ameambiwa nafasi atapata mwezi wa pili mwaka huu sasa nataka apate sehemu ya kujishikiza kwa muda angalao mpaka hiyo tarehe 15.02.2015 atakapopata nafasi ya wizara kufanya intern.
Naomba mnisaidie kwa hili.
Ahsante.
 
leo ni tarehe 28/1/2015 bado siku 7 , kwa hiyo subili aanze intenship huko alikopamgiwa mpatie pesa ya kuanzia baadaye atakuwa vizuri kipesa
 
Ok ndugu Mbalila najua bado takriban wiki mbili kuanza kazi yeye ila ombi langu ni kwamba hata kwa huu muda mfupi kwa level aliyonayo nimefikiri anaweza kufanya jambo la kuonekana kwa kujishughulisha kwa namna fulani. Ndiyo maana nikaja kwenu kuomba kama kuna sehemu yoyote mtu anajua kuwa panaweza kumsaidia huyo kijana asikae tu asubuhi hadi jioni bure na elimu yote hiyo.
 
Jamani wiki 2 ni chache Sana, bajeti hata chips dume kilo tosha kabisa unless Kuna lingine???
 
Acha ubahili muhudumie tu mungu atakulipa bado wk 2 tu atakua vzr
 
Wiki mbili ni chache sana ndugu kuwa na moyo wa uvumilivu unampomsaidia ndugu yako inavyoonekana ni ndugu yako wa karibu sana. Sisi wengine timesomeshwa na ndugu tu kutoka A level hadi degree wewe ungeweza . Ungefikiria hiyo internship akiwa anakaribia kutoka chuo aanze kuapply for internship. La mwisho nani atakubali amuajiri mtu for a contract of two weeks.
 
jamaa noma two weeks anaona nyingi wakati watu wana miaka mitatu. duh vumilia kaka cyo nyingi
 
Watu wengine mpaka Leo hawana ajira zaidi ya miaka 3 na wanalishwa,valishwa Nk lakini hawatutengi hivyo
 
Back
Top Bottom