Msaada: Hivi "degree" ni nini?

kkarumekenge

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
1,708
1,026
Watu husoma na kusoma hadi tunaambiwa wamepata "degree", napenda kufahamu kwa kutunukiwa hiyo "degree" huwa wamepata nini haswa. Maana tunasikia tu huyu ama yule ana "degree", ndo kuwa na nini?
 
Mkuu, endelea kusubiri tu watalaam watakupa majibu, hata kama ungeuliza kuhusu PHD naamini majibu yanapatikana humu humu.
 
Degree ni kizungu, kwa kiswahili ni nyuzi. SI Unit ya Degree ni Centigrade ama Fahrenheit, umeelewa kaka?
 
degree ni kiwango cha elimu kinachozidi higher diploma..
 
Kwa tafsiri ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education-NACTE) Degree (Shahada) ni ni kiwango cha elimu kinachozidi ya upili (secondary) LAKINI chenye kumbainisha mwenye nayo kama anayeweza kutoa majibu kwa matatizo yanayomzunguka.

NACTE hutunuku Madaraja mbali mbali ya elimu na degree huanzia NTA 8. Sasa NTA zote ni hizi hapa na kirefu cha NTA=National Technical Award
1. NTA 4-Basic Technician Certificate

2. NTA 5- Technician Certificate

3. NTA 6- Ordinary Diploma

4. NTA 7-Advanced/Higher Diploma

5. NTA 8-Bachelor's Degree

6. NTA 9-Masters Degree

7. NTA 10-Doctorate Degree. (Philosophy Doctor-PhD)

Kwahio degree zinaanzia namba 5 yaani NTA 8 na zipo aina Tatu mpaka NTA 10.

Ukijiuliza mbona kwenye mtiririko hakuna NTA 1, 2 na 3 jibu ni kwamba hizo hutolewa na Mamlaka ya Taifa ya Elimu ya Ufundi (Vocational Education Training Authority-VETA) na haziitwi NTA bali NVA yaani National Vocational Awards. NVA 1 ndio Trade Test 3, NVA 2 ndio Trade Test 2 na NVA 3 ndio Trade Test 1. Kumbuka Trade Test 1 ndio ya juu zaidi kwa VETA na ndio hio huitwa NVA 3 kisha ndio huanza NTA za NACTE.

NB:Nilipokosea nirekebishwe
 
Back
Top Bottom