Niliwahi kusimuliwa hadithi moja na mama yangu sisi ni wakristo lakini katika kupanga panga siku moja mama alikuta kitabu cha kiislamu kufungua ndani akakuta hadithi moja inasema hivi kuna mtu na mwanawe walikuwa maskini sana walikuwa waliishi nje, mbali ya mji ili ufike kwenye mji ni lazima upite kwenye pori. Kazi ya yule mtu na mwanae ilikuwa kujidamka na kwenda mjini kuomba na kurudi nyumbani. Kila siku walifanya hivyo lakini mara nyingi kama si mara zote waliambulia patupu. Siku moja wakati wakivuka lile pori yule baba maskini akawaza 'kwa nini nisikate kuni wakati naomba kwenye kijiwe changu nitaziweka niuze'?, basi akakata mzigo kiasi tu akaubeba ile kuingia mjini tu akasikia kunii we mzee mwenye kuni leta, akauza zile kuni wakanunua unga wakarudi nyumbani kesho yake wakakata kuni nyingi zaidi ikawa hata kabla ya kufika kijiweni kuni zinakuwa zimekwisha. Walibadili maisha yao kwani walikuwa wauza kuni maarufu kwenye maharusi, shule na matumizi ya nyumbani.Jamani sote kuna wakati tumepitia magumu yasioandikika lakini KUOMBA NI MWIKO.