MSAADA: HATUA NA TARATIBU ZA KUWA REFEREE (Football)

GREGO

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
4,279
2,921
Kuna rafiki yangu anapenda kujua taratibu na hatua za kupitia hadi kuwa referee wa mpira wa miguu. Naomba kujuzwa ili nimpe jibu wanaJF

Naomba kuwasilisha.
 
aende pale tff atapewa majibu sio kilakitu spoon feeding mwisho atadanganywa bure maana humu kuna watu kila kitu wanajua wao
 
Ameshachelewa. Urefa unaanza toka chekechea, shuleni, sekondari, nk. Kila wenzako wakicheza wewe unakuw refa. Ni hobi ya kufanya maamuzi ya mpira wa miguu. Unajenga uzoefu kwa muda mrefu, unatambulika toka ligi za mchangani, wilayani, ngazi ya mikoa hadi taifa. Si kazi ya kuajiriwa bali ni ya kujitolea, hata ulaya urefa si kazi. Kila mechi unayochezesha unalipwa posho na kuondoka. Unatakiwa uwe na fani yako na kazi yako. Kama hujachezesha mechi yoyote na umeshamaliza masomo mpaka sekondari sahau kuwa refa. Kwa sababu tayari huna hobi na hujashiriki michezo na mpira wa miguu kwa muda mrefu mpaka umezeeka.
 
Natanguliza shukrani zangu kwako Mkuu kwa ufafanuzi ila huyu jamaa ni mchezaji wa mpira sema yuko kijijini sana na hua anachezesha mechi za kombe la mbuzi na kuku na ana hobi ndo maana kauliza
 
Back
Top Bottom