Tofauti ipo tena kubwa sana
Kosa la kuiba ni pale ambapo mshtakiwa alidhamiria kuiba na akafanikiwa kuiba kitu hiko na endapo atapatikana kosa hilo basi kwa mujibu wa kanuni ya adhabu kifungu namba 265 mtu huyo atahukumiwa adhabu ya miaka 7
Kukusudia kuiba ni pale mtu anapodhamiria kuiba na katika kitendo kile cha wizi bac akashindwa kutekeleza adhma yake ya kuiba labda alikutwa au kitu kngne chochote kilimzuia kutekeleza japo alidhamiria kwa asilimia 100 kuiba na endapo atapatikana na kosa hilo basi ataadhibiwa kifungo cha miaka miwili au fain au vyote kwa pamoja kwa mujibu kanuni ya adhabu kifungu namba 380.