Msaada: Habari za Robert Yakobo Sangwani, Fundi wa Kimataifa

Steven Sambali

JF-Expert Member
Jul 31, 2008
352
170
Wana Mtandao,

Kuna ombi kutoka kwa aliyekuwa Balozi (Konsula) wa Ubalozi wa Poland nchini Tanzania Prof. Augeniusz Rzewulski kanitumia ujumbe akiomba msaada wa kupata habari za huyu Msanii maarufu wa zamani nchini Tanzania, Fundi wa Kimataifa - Yakobo.

Huyu Msanii sanamu zake za kimakakonde alizokuwa akichonga kwenye shina la mti wa Mpingo ndiyo zilizokuwa zikipewa wageni wengi wanaokuja Tanzania.
Hata Obama alipokuja alipewa sanamu kama hiyo ingawa yeye Yakobo alishafariki ila ufundi wake hadi leo unaendelezwa na hao aliowaacha hadi leo wanachonga au kumwiga.

Mwenge siku moja nilibahatika kuziona kwa karibu na Archtect Chagula alianza kuzisifia hadi nikavutiwa na kuanza kuziangalia kwa karibu. Akaniambia nichukue picha kadhaa za hizo sanamu ambazo hadi leo ninazo. Kama siyo huyo Chagula basi nadhani nisingelikuwa na habari yoyote kuhusu hizo sanamu. Ni Mzee Rzewulski ndiye kaja kuniambia mwanzilishi huyu.

Prof. Rzewulski akiwa Tanzania bado ubalozini, alibahatika kuwasiliana naye na akamuomba amchongee sanamu moja. Kuna uwezekano mkubwa ndiyo ilikuwa sanamu yake ya mwisho ambayo hadi leo anayo hapa Poland. Baadaye alijulishwa amefariki na akafika kutoa pole na rambirambi kwa familia yake Fundi Yakobo. Hii ilikuwa mwaka 1996.

Kwa mapenzi makubwa aliyonayo kwake, mwezi wa nne ameamaua kufanya maonyesho ya Marehemu Yakobo na hasa sanamu zake ziitwazo UJAMAA.
Kama kuna mtu ana habari ni wapi naweza kuwasiliana na kupata habari zaidi, picha, Audio, Film nk basi itakuwa vema sana kufanikisha maonyesho hayo na wakati huo huo kutangaza jina la nchi kwani Watanzania tumekuwa tukilalamika Wakenya kutangaza vivutio vyetu vya utalii wakati sisi wenyewe hatufanyi hivyo.

Kama kuna mtu ana Email ya nyumba ya Makumbusho, Nation Museum, wafanyakazi wa TBS, Radio Tanzania, Michuzi Blogs, Mjengwa, Manyerere Jackton, Jasusi na waandishi wengine wengi na watu wa historia au waliobahatika kumfahamu, basi naomba msaada wenu.

Natanguliza asante. Mungu Ibariki Tanzania.

Majibu niandikie hapa JF au nitumie email: Ssambali@hotmail.com
 
Ujumbe kwa ufupi kutoka kwa Prof. Rzewulski baada ya kuutafasiri kwenye lugha ya Kiingereza. Mtu anaweza kuandika hata kwa Kiswahili kwani Prof. ni Mwalimu wa Kiswahili hapa Warsaw University hivyo atasoma bila wasiwasi. Kiingereza itakuwa vema zaidi kwani ntamtumia kama ujumbe ulivyo na wengi wanaweza kuuweka kwa Kipolish.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Dear Steve,
in reference to our conversation, I am looking additional information on Robert Yakobo Sangwani.
- First of all, I need several photographs Yakobo and consent of the authors (or trustees) for their show at the exhibition.
- Photographs of his sculptures by the collections in Tanzania.
- List of exhibitions for whom his works were shown.
- Also information about the life of Yakobo - some memories of people who knew him on reviews on his arts.
- Probably Radio Tanzania or other Radios has some recordings of the voice of Yakobo in Swahili language eventually in English language.
- Maybe television in Tanzania.

Any help will be recorded in the materials of the exhibition, including its directory.

Ahsante sana,
Eugeniusz Rzewuski
 
Wasanii watunukiwa tuzo Siku ya Msanii

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

WASANII wanne wa sanaa mbalimbali nchini juzi wametunukiwa tuzo maalumu katika usiku wa tuzo za wasanii zilizofanyika katika ukumbi wa Nyumba ya Sanaa, Posta Dar es Salaam.

Tuzo hizo zilitolewa na Katibu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii, Elisante Gabriel, huku ikihudhuriwa na wasanii mbalimbali.

Tuzo ya kwanza ya heshima ya sanaa za maonyesho ilikwenda kwa mwigizaji mkongwe nchini ambaye michezo yake ilikuwa ikisikika kwenye redio Tanzania enzi hizo, Bakari Mbelembe ‘Mzee Jangala’.

Tuzo ya sanaa ya ufundi ilikwenda kwa Robert Yakobo ‘Sangwani’ huku tuzo ya heshima katika filamu akitunukiwa Thecla Mjata na Tuzo ya heshima katika muziki ilikwenda kwa mwimbaji mkongwe wa muziki wa mwambao, Shakira Said ‘Bi Shakira’.

Akizungumza kabla ya kukabidhi tuzo hizo, Katibu huyo alisema ufike wakati wasanii watambue thamani yao na sio kujirahisisha kitendo kinachowafanya kuonekana ni rahisi.

“Nyie mna thamani kubwa sana, msijirahisishe kwa kufanya kazi za bei rahisi ambazo haziendani na thamani yenu mtakuwa hamjitendei haki na kuzidi kushusha thamani ya sanaa nchini.

“Serikali imetambua mchango na umuhimu wenu na ndiyo maana kuna mabadiliko makubwa yaliyofanywa kwenye wizara hii kwa kuwekwa wasanii kitu ambacho hakikuwepo, sasa tunataka kuona nanyi mnalitendea haki Taifa, nidhamu ni jambo la msingi na linapaswa kufuatwa lakini pia masuala yenu muyamalize wenyewe sio kitu kidogo mnakimbilia vyombo vya habari, mnajiharibia sifa,” alisema Gabriel.

Usiku huo ulipambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa kundi la ngoma za asili na sarakasi la Dar Creative, Msanii wa kuigiza sauti za wasanii mbalimbali na watu maarufu, Mlugaluga pamoja na bendi ya K-Mondo Sound.

From: Wasanii watunukiwa tuzo Siku ya Msanii
 
Sanamu ya Ujamaa ikiwa ofisini/nyumbani kwa Obama huko USA.

o-OBAMA-SPIDERMAN-570.jpg
 
Bado sijapata jibu wala habari yoyote hadi leo hii. Nakumbusha tu ombi langu.
 
Kwa nini usitafute web ya makumbusho ya taifa?
Mkuu Tokomea,
Asante kwa kuwa wa kwanza kujibu. Nimejaribu kutafuta Website ya Makumbusho ya Taifa nimeshindwa kuipata hata email yao pia sina. Pia kwa bahati mbaya sipo Dar es salaam na hivyo inakuwa ngumu kwangu kwenda kuwaulizia.

Nilitegemea kuna mtu anamfahamu mhusika hata mmoja na hiyo itakuwa njia rahisi kuwafikia wahusika.
 
Thread kama hizi watu wanapita kimya kimya ni ajabu. Umekwisha pata mawasiliano yoyote ya kuanzia?
Mkuu huwezi kuamini kuwa hadi leo wewe ni mtu wa pili walau unaandika.

Nashindwa kuamini kuwa jamaa ameshasahaulika kiasi hicho wakati sanamu zake wamepewa viongozi mbalimbali duniani.

Hata kupata email ya Makumbusho ya Taifa pia nimekosa. Ni kama hivi vitu havipo kabisa Tanzania.

Nazidi kusubiri labda kuna mtu atajitokea kuniandikia.
 
FAMILY TREE KNOWN AS UJAMAA in Kiswahili by MTO WA MBU Northern Tanzania Makonde Woodcarvers pt 2.m4v



Source: ruudmom's channel youtube


MAKONDE CURVERS MWENGE DSM

A video about the Makonde Carvers of Mwenge, Dar-es-Salaam 2006



Source: George Lilanga Lilanga - Makonde - Tingatinga

N.B
Ukijaribu kuwasiliana na source wa hizi video clip utaweza kupata habari zaidi

  1. George Lilanga : Click here: Lilanga - Makonde - Tingatinga & makonde@t-online.de
  2. ruudmom's channel youtube
  3. Masters of the Makonde movement include Thomas Valentino (Binadamu), Robert Yakobo Sangwani (Ujamaa), Clement Ngala (Mawingu), John Fundi and George Lilanga (Shetani). Read more: http://allafrica.com/stories/201409181153.html
 
Mkuu Mwanagenzi,

Samahani nilipitiwa kidogo na vikazi na kama siku 3 nilikuwa sijaupitia huu uzi.

Nishamuonyesha huu uzi Profesa Rzewulski na ntamjulisha kwa kumwandikia hii email uliyotutumia.

Nashukuru sana kwa kulifuatilia hili swala hasa ukichukulia tumekuwa tukilalamika kuwa Wakenya wanatuibia.

Ntakujulisha majibu tuliyoyapata mara nikishapata habari kamili.

Mungu Ibariki Tanzania.

Pole sana.

Jaribu kumwandikia email huyu ndugu: aumabu@gmail.com.

Baadaye tupe mrejesho wa hayo maonyesho.
 
FAMILY TREE KNOWN AS UJAMAA in Kiswahili by MTO WA MBU Northern Tanzania Makonde Woodcarvers pt 2.m4v



Source: ruudmom's channel youtube


MAKONDE CURVERS MWENGE DSM

A video about the Makonde Carvers of Mwenge, Dar-es-Salaam 2006



Source: George Lilanga Lilanga - Makonde - Tingatinga

N.B
Ukijaribu kuwasiliana na source wa hizi video clip utaweza kupata habari zaidi

  1. George Lilanga : Click here: Lilanga - Makonde - Tingatinga & makonde@t-online.de
  2. ruudmom's channel youtube
  3. Masters of the Makonde movement include Thomas Valentino (Binadamu), Robert Yakobo Sangwani (Ujamaa), Clement Ngala (Mawingu), John Fundi and George Lilanga (Shetani). Read more: http://allafrica.com/stories/201409181153.html

Bagamoyo,

Nashukuru sana kwa nondo zako. Ngoja nimjulishe Prof. aje hapa ajisomee mwenyewe maadamu anafahamu Kiswahili.

Nafikiri umeweka nondo za kutosha na hasa hiyo ya German maana wanaweza kuwa na habari nyingi sana hawa jamaa.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom