Msaada: Gharama za kuvusha gari kutoka Zanzibar kuja Dar

Matendo Andrew

JF-Expert Member
Apr 1, 2014
748
366
Nikihitaji kuvusha gari taka Zanzibar kuja Tanzania bara kwa kutembelea kwa mwezi mmoja utaratibu upoje na gharama zake?

Msaada wakuu. Asante.
 
Utaratibu ni kwamba inaruhusika,na utapewa kibali cha muda kama sikosei ni miezi mitatu tu.
Na wala hautalipia Tax kama gari nyingine ambazo zinavushwa Dar moja kwa moja na kusalia huko.
Ila Number za Zanzibar ndio utakazo zitumia.
Hapo unalipia tu,Usafiri wa Meli ya Kuvusha na TRA ili kupata kibali,maana ukikamatwa na Majembe watakuzingua tu,halafu pia Traffic ili upewe Permit maalum.
Maana hilo hata wa South Africa wengi wanakuja na Gari zao wale walio kwenye Overland trips na hata wakenya wengi sana wanakuja na Gari zao Dar na kugeuza nazo.
Ila zaidi kama una ndugu Dar mwambie aende TRA na Traffic makao makuu atapewa muongozo ili ajue aanzie wapi.
 
Kwa zanzibar bora ukodi tu tax,itakamatwa mpaka itoke mwezi,watataka uthibitisho kuwa umekuja kutembea na sio kuliuza
Ni wamajeshi tu ndio wanaweza kuvuka nayo
 
Hahahaha,hili nalo ni tatizo.
Maana gharama tu ya kulileta huko na kurudi ni kubwa mno,
na Usalama watahoji kwamba umeenda nalo kuliuza,na huu mchezo umekuwa ukifanyika sana.
Maana matajiri wote gari wanaziacha,sasa wewe kigari cha milioni 10 au 20 utumie gharama zaidi ya 2m kwa kutembelea Dar tu na kurudi.
Watahofu kwamba unaenda kupiga dili la kuliuza au ujambazi
 
Mwaka jana nililipa laki 2 na themanini na kwakuwa ilikuwa imelipiwa us huru wote Nilitoa laki 5 tu ya clearing und fording
 
Wadau nikitaka kununua Gari toka Zanzibar ntalazimika kulipia kiasiki gn km ushuru pamoja na registration ya namba za huku bara?...hapa pia naona kunachangamoto ya kisiasa jamuhuri moja plate number tofauti?!!
 
Back
Top Bottom