Fuata njia zifuatazo ili kufungua flash yako iliyo HIDE files ndani yake:
1.Chomeka flash husika ktk computer yeyote mradi tuu iwe inatumia OS ya windows 7 au 8/8.1 (Na njia hii inatumika hata kwa windows xp japo hapa nitatoa maelezo kwa windows 7 au 8/8.1)
2.Fungua windows explorer (Yaani pale palipozoeleka kama my computer) na usome drive letter iliyopo katika flash husika. Drive letter ni ile herufi inayoandikwa mbele ya jina la flash yako au zile partition za Hard Disk ya computer.mf: Removable Disk (F) hapa drive letter ni F. Hivyo note down flash yako itakuwa na herufi gani kwan ukichanganya na hard disk ya PC hatutafanikiwa chochote hapa.
3.Bonyeza alama ya start (Windows logo) alafu andika pale kwenye search box neno 'CMD' (bila hizo quotes)
>Kisha utaona CMD katika ulivyo search, sasa click hapo kuifungua. Itafunguka box leusi lenye maneno C:\user...>\ _
na cursor inayo blink kumaanisha unatakiwa kuandika kitu.
4.sasa andika ifuatavyo bila kukosea
attrib -s -r -h /s /d G:\*.* alafu bonyeza enter.
..Sasa ngoja nitafsiri jinsi ya kuandika hizo code hapo kwani ukikosea kidogo tuu command hii haitafanya kazi,
Ipo hivi: ukishaandika "attrib" weka nafasi alafu ndo uandike -s then weka nafasi andika -r then nafasi tena andika -h then nafasi tena andika /s (yaan kati ya / na s hakuna nafasi) alafu kutoka /s kuja slash (/) ya pili weka nafasi (yaani hivi /s /) Again baada ya slash iliyombele ya s andika /d (yaan hapo usiweke nafasi kati ya / na d, then weka nafasi kisha andika drive letter ya flash yako..mimi nimeandika G kama vile ndio flash yangu, then weka alama za Semi-colon mbele tu ya drive letter yako (G🙂 then weka back slash ikifuatiwa na nyota,nukta na nyota bila kuweka nafasi kati yao (yaan hivi G:\*.*) baada ya hapo bonyeza ENTER na usubiri hadi uone yale maneno yaliyokwepo tangu mwazo kabla hatuja andika chochote katika cmd yetu yamerudi ambayo yalikuwa ni C:\USER\....>\
5.Ikiwa uliandika command hii kiusahihi basi rudi kwenye flash yako ifugue utakuta folder moja lisilo na jina mbele yake, then lifungue hilo na humo ndani utakuta vitu vyoteee.
Njia hii hutumika pia kufungua flash iliyo pigwa shortcut...yaan unakuta flash ukiifungua inakuwa na kishortcut kimeandikwa jina la flsh kama hivi "Removable disk (G)"
Siku njema!