Msaada: External hard drive ya 1 TB sasa inasoma GB 60

Msaada: External hard drive ya 1 TB sasa inasoma GB 60

korokwincho

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2014
Posts
1,071
Reaction score
1,318
Wakuu habari za saa hizi, Mimi mwenzenu kuna mtu alitoka nje (Netherlands) akaniletea external HDD ya samsung model no. NM-0810 ambayo ni 1TB ambayo hata nilivyoichomeka kwa Mara kwanza kwenye PC yangu ilisoma 934 GB na nikatuma zaidi ya files za movies GB 300 kwenye hiyo external lakini nilipoichukua na kuweka kwenye smart TV yangu iligoma kusoma cause file system ilkuwa ni exfat mpaka nilipoiformat kwa FAT32 ndio ikakubali kusoma lakini cha ajabu size yake ilipungua sana mpaka sasa inasoma GB 60 tu kwenye PC karibuni 3 tofauti, naombeni msaada wenu hapo wa kurudisha size ya external kama awali maana nimeshaiformat tena na tena lakini wapi, natumia windows 8.1.

Asanteni
 
Cheki software za kufanyia partition huwenda imeingia partition na storage nyengine hujaispecify itumikeje.

Tumia hata mini tool partition wizard inaweza fanya kazi hio
 
Okay asante mkuu mkwawa nitajaribu hyo njia umeme ukirudi
 
Ukiona maelezo ya Chief-Mkwawa yamegoma mkuu soma hapa chini,

Unazijua hizi za kwenye picha,, Uki-format tu zinarudi kwenye kwenye size yake ya flash, ni fake hard drive mkuu, kama ulituma data kubwa na umeiformat ikapungua kabisa yaweza pia ikawa unakitu kama hiki ndani na sio Hard Disk Case ni ka USB drive kafungwa vizuri,

fake2.jpeg

Ndio kwa mara ya kwanza ukituma file hata GB 500, itajifanya imepokea kumbe imechukua file names tu na extension zake. Ukiiformat tu , kwisha habari yake

Ichunguze vizuri Hard Disk yako,
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom